WAZIRI wa Maji Proffesa Makame Mbarawa akizungumza wakati akizundua bodi mpya ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) ambapo pia aliwataka kufanya kazi kwa uwazi isipokuwa pale mahitaji ya kisheria yanapolazimisha vinginevyo
MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza wakati wa halfa hiyo
Mwenyekiti Mpya wa Bodi ya Tanga Uwasa Dkt Fungo Ally akizungumza wakati wa uzinduzi wa bodi mpya
MKURUGENZI wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly akizungumza wakati wa uzinduzi wa bodi mpya
MKURUGENZI wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly kushoto akiteta jambo na Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa wakati wa uzinduzi huo
WAZIRI wa Maji Proffesa Makame Mbarawa kulia akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kushoto wakati wa uzinduzi wa Bodi mpya ya wakurugenzi wa Tanga Uwasa kulia ni Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Salum Shamte kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Shekifu
WAZIRI wa Maji Proffesa Makame Mbarawa kushoto akifurahia jambo na Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly wakati wa uzinduzi wa Bodi Mpya ya Tanga Uwasa
Sehemu ya wageni waalikwa kwenye uzinduzi huo
Watumishi wa Tanga Uwasa wakimsikiliza Waziri wa Maji Proffesa Makambe Mbarawa kulia ni PRO wa Tanga Uwasa Dorrah Killio
Watumishi wa Tanga Uwasa wakimsikiliza Waziri wa Maji Proffesa Makambe Mbarawa
Sehemu ya waalikwa wakiwa kwenye uzinduzi huo
WAZIRI wa Maji Proffesa Makame Mbarawa kulia akigawa vifaa vya utendaji kwa wajumbe wapya wa Bodi hiyo Mhandisi Zena Saidi ambaye ni Katibu Tawala wa mkoa wa Tanga
WAZIRI wa Maji Proffesa Makame Mbarawa kulia akigawa vitendea kazi kwa Mwenyekiti Mpya wa Bodi ya Tanga Uwasa Dkt Fungo Ally kulia ni Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly
WAZIRI wa Maji Proffesa Makame Mbarawa amewataka wajumbe wa bodi ya wakurugenzi ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) kuepuka mgongano wa kimaslahi katika utekelezaji wa majukumu yao.
Proffesa Mbarawa aliyasema hayo wakati akizundua bodi mpya ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) ambapo pia aliwataka kufanya kazi kwa uwazi isipokuwa pale mahitaji ya kisheria yanapolazimisha vinginevyo
“Lakini matumizi sheria hii ya maji yaambnatane na matumizi ya sheria nyengine katika uendeshaji wa taasisi za umma kufikia dhana nzima ya utawala bora mfano sheria ya manunuzi ya umma, sheria ya mazingira, sheria ya fedha “Alisema Waziri Mbarawa.
“Pia bodi mhakikishe hesabu za mamlaka zimeandaliwa kutunzwa kwa usahihi kulingana na mifumo wa kimataifa wa ripoti za fedha (International Public Sector Accountin Standards (IPSAS).
Awali akizungumza Mwenyekiti kwa niaba ya Bodi ya Wakurugenzi waliomaliza muda wao Salum Shamte alisema kwamba mafanikio yaliyopatikana wakati wao ni pamoja na kuendelea kutoa huduma bora kwa wateja wa maji safi na majitaka ,kuboresha mipango,bajeti na utendaji ikiwa ni pamoja na kupata hati safi za mahesabu kila mwaka.
Alisema pia wamesaidia kuiwezesha mamlaka kuongeza mashine mbili za vifaa vya kupunguza matumizi ya umeme kwenye mtambo mkubwa wa kusukuma maji eneo la Mabayani ambapo vifaa hivyo vimepunguza gharama kwa kati ya asilimia 10 hadi 15 kwa mwezi
“Lakini pia kusimamia kuhuisha mkataba kati ya Tanga Uwasa na Taasisi ya wananchi wa Muheza ya Uwamakizi wa kutunza vyanzo vya maji yam to Zigi wa Shilingi milioni 180 kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia Novemba 2016 hadi 2019”Alisema
Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly alisema kwamba mtandao wa maji taka unapatikana kidogo sana na wapo asilimia 9.7 kwa eneo la mjini huku akieleza changamoto ya kupasuka kwa mabomba za maji taka zimekuwa zikijitokeza mara kwa mara.
Naye kwa upande wake Mwakilishi wa Wafanyakazi wa Mamlaka hiyo Fransis Barabara alisema kwamba katika kipindi cha bodi iliyomaliza muda wake wameshuhudia upanuzi wa mtandao wa majisafi ukienda sambamba na ongezeko la wateja hali iliyoweza kuongezeka kwa mapato ya mamlaka kwa ujumla ukilinganisha na hapo awali.
Alisema pia kodi kwenye mishahara na posho mbalimbali imeendelea kuwa juu na kuathiri maisha ya watumishi kimapato licha ya kupigiwa kelele na wadau mbalimbali wa sekta za ajira bado suala hili halijapatiwa ufumbuzi na hivyo kufanya washindwe kumudu makali ya maisha.
“Sheria ya utumishi wa umma na 8 ya mwaka 2002 inaelekeza mtumishi wa umma kulipwa posho isiyo na makato ya kodi lakini kwa Tanga Uwasa bado posho za watumishi zinaendelea kukatwa kodi “Alisema