Home Burudani MSANII WA BONGOFLEVA DESMOND (GOLDEN BOY) KUCHOMOZA NA “TUNAKESHA”

MSANII WA BONGOFLEVA DESMOND (GOLDEN BOY) KUCHOMOZA NA “TUNAKESHA”

0

Kijana Steven Michael Desmond “Golden Boy” anayeimba muziki wa kizazi kipya (Bongo Fleva)amesema anakuja na kibao kipya cha “Tunakesha” kinachokwenda kwa mtindo wa Afripop, Desmond amesema hii ni nyimbo yake ya kwanza na anatarajia kuiachia wakati wowote, Kaa mguu sawa.

Amesema amejipanga na anaamini kibao chake kitapokelewa vizuri na mashabiki wa muziki wa kizazi kipya (Bongofleva) pamoja na kwamba yeye ndiyo kwanza anaingia kwenye muziki wa kizazi kipya ambao una wasanii wengi wakali na wenye ushindani mkubwa.

Amesema amejizatiti vyema kuingia katika anga za Bongo Fleva ninachoomba ni mashabiki kunipokea kwa mikono miwili ili waone ubora wa kazi yangu na nina imani wataukubali.

“Ninakuja nipokeeni kwa mikono miwili nina imani nitawapa burudani nzuri itakayowavutia sana” Amemaliza Desmond.