Home Mchanganyiko RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN AZUNGUMZA NA UONGOZI WA WIZARA YA BIASHARA...

RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN AZUNGUMZA NA UONGOZI WA WIZARA YA BIASHARA NA VIWANDA ZANZIBAR

0

WAZIRI wa Biashara na Viwanda Zanzibar Mhe. Balozi Amina Salum Ali akiwasirisha mutasari wa Utekelezaji wa Bajeti na Mpango Kazi wa Wizara yake kwa mwezi wa Julai 2018 hadi Juni 2019, kulia Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Abdulhamid Yahya Mzee na kushoto Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda Zanzibar Mhe. Hassan Khamis Hafidh, uliofanyika ukumbi wa Ikulu Zanzibar ukiongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, hayupo pichani.(Picha na Ikulu).

MKURUGENZI wa Taasisi ya Viwango Zanzibar  (ZBS)  Ndg .Khatib Mwadin  akijibu swali wakati wa mkutano wa Utekelezaji wa Bajeti ya Mpango Kazi kwa mwezi Julai 2018 hadi Juni 2019, uliofanyika ukumbi wa Ikulu Zanzibar, ukiongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, (hayupo pichani  kulia Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Biashara Zanzibar (ZSTC) Dk. Said Seif Mzee (Picha na Ikulu).

MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali Iddi akizungumza wakati wa mkutano wa Utekelezaji wa Bajeti na Mpango Kazi wa Wizara ya Biashara na Viwanda Zanzibar kwa mwezi Julai 2018 hadi Juni 2019, uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu) .

NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Biashara na Viwanda Zanzibar Bi. Khadija Khamis Rajab wa kwanza kushoto akisoma taarifa ya Utekelezaji Bajeti na Mpango Kazi ya Wizara yake kwa mwezi wa Julai 2018 hadi Juni 2018, wakati wa mkutano huo uliofanyika Ukumbi wa Ikulu Zanzibar ukiongozwa na Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein.(Picha na Ikulu).

MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC) Ndg Maalim Kassim Suleiman, akizungumza wakati wa mkutano wa Utekelezaji wa Bajeti na Mpango Kazi wa Wizara ya Biashara na Viwanda kwa mwezi wa Julai 2018 hadi Juni 2019, uliofanyika ukumbi wa Ikulu Zanzibar, ukiongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, hayupo pichani.(Picha na Ikulu)