Home Biashara MASHIRIKA YATOA ELIMU YA LISHE BORA KWENYE MBIO ZA MWENGE NZEGA TABORA

MASHIRIKA YATOA ELIMU YA LISHE BORA KWENYE MBIO ZA MWENGE NZEGA TABORA

0

 

Mwananchi aliyefika kutembelea banda la mashirika mawili ya yasio ya kiserikali ya Save the Mother and Children of Central Tanzania (SMCCT) la mkoani Singida na Christian Education and Development Organization (CEDO) la mkoani Tabora, akielezea kufurahisha na elimu ya masuala ya lishe kwa mama mjamzito iliyotolewa na mashirika hayo kwenye mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani Nzega mkoani Tabora jana . Kulia ni Mkurugenzi wa Shirika la CEDO, Japhet Kalegeya na katikati ni Mkurugenzi wa SMCCT, Eveline Lyimo. 
Maonyesho yakiendelea.
Na Dotto Mwaibale, Nzega. 
MASHIRIKA Mawili yasio ya kiserikali ya Save the Mother and
Children of Central Tanzania (SMCCT) la mkoani Singida na Christian Education
and Development Organization (CEDO) la mkoani Tabora yametoa elimu kwa jamii
kuhusu lishe bora kwa mtoto ikiwemo suala la elimu, afya na ulinzi wa mtoto
Wakati wa monyesho ya viazi lishe katika hafla ya kuupokea Mwenge wa Uhuru
Wilayani Nzega, Mkoani Tabora.
Maofisa wa taasisi hizo wakitoa  elimu kwa jamii juu ya haki ya mtoto kupata
lishe bora katika maonyesho ya bidhaa zitokanazo na viazi lishe kwenye mbio za
Mwenge wa Uhuru wilayani hapa juzi
walisema mtoto anapaswa kupata lishe hiyo yenye virutubishi kama viazi
lishe na kula vyakula vya aina mbalimbali tangu akiwa tumboni mwa mama yake.
Mkurugenzi  Mtendaji
wa Shirika la Save Mother and Children Central of Tanzania (SMCCT ) Evaline
Lyimo alisema lishe bora kwa ntoto uanzia tangu akiwa tumboni mwa mama yake.
” Lishe bora inasaidia kuboresha ukuaji wa mtoto
kimwili na kiakli,  kupungua uwezekano wa
kupata mtoto mwenye uzito pungufu na kupunguza udumavu”
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la CEDO, Japhet Kalegeya
alisema vyakula vya aina mbalimbali na vyenye virutubisho vinahitajika sana
katika ukuaji wa mtoto na ndio maana huwa wanamsisitiza mama mjamzito kuvitumia
na kupata muda wa kupumzika.
“Tumekuwa tukisisitiza sana matumizi ya vyakula hivyo
kwa mama mjamzito jambo linalosaidia mtoto akizaliwa kuwa na afya njema na
kumuepusha na utapiamlo na ugonjwa wa manjano” alisema