Home Uncategorized MKOA WA PWANI WAPATA KIWANDA CHA KISASA KWA AJILI YA KUCHAKATA ZAO...

MKOA WA PWANI WAPATA KIWANDA CHA KISASA KWA AJILI YA KUCHAKATA ZAO LA MUHOGO

0

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarest Ndikilo kushoto akipeana mkono wa pongezi na Mkurugenzi mtendaji wa  kiwanda cha kuchakata zao la  muhogo mara baada ya halfa ya kuweka jiwe la msingi katika kiwanda hicho amabcho kimejengwa katika kijiji cha Mgenge kata ya Beta Wilayani Mkuranga,(PICHA NA VICTOR MASANGU).

Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani kushoto Ramadhani Maneno akimshika mkono Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo ikiwa ni moja ya ishara ya kumpongeza katika juhudi zake za kuunga mkono juhudi za serikali katika ujenzi wa viwanda(PICHA NA VICTOR MASANGU).

Mmoja wa viongozi wa kiwanda hicho cha kuchakata zao la muhogo kulia  Leonard Jambeli akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi huo kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani kabla ya uwekaji wa jiwe la msingi katika kiwanda hicho pembeni yake kushoto ni Mkurugenzi mtendaji wa kiwanda hicho(PICHA NA VITCOR MASANGU

Mkuu wa Mkoa wa Pwani kushoto Mhandisi Evarist Ndikilo akipata maelekezo kutoka kwa mkurugenzi mtendaji wa kiwanda cha kuchakata muhogo wakati alipofanya ziaara yake ya kikazi kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi katika kiwanda hicho,(PICHA NA VICTOR MASANGU).

*****************

VICTOR  MASANGU, MKURANGA

KILIO cha muda mrefu ambao kilkuwa kinawakabili wakulima wa zao la muhogo katika Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani hatimaye hivi karibuni  wanatarajia   kuondokana na changamoto sugu ya upatikanaji wa soko la uhakika   kufuatia kuanza  kwa  ujenzi wa mradi  wa kiwanda kikubwa cha kuchakata zao hilo  ambacho kitagharimu kiasi cha shilingi bilioni 9.5

Hayo yamebainishwa na baadhi ya wakulima hao wakati wa Ziara ya kikazi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo wakati wa halfa ya uwekeaji wa jiwe la msingi katika kiwanda hicho ambacho kimejengwa na mwekezaji kutoka nchini China katika kijiji cha Mkenge  kata ya Beta Wilayani Mkuranga ambapo wamedai hapo awali walikuwa na tatizo la kuuza mihogo yao  kwa bei ya hasara.

“Sisi kama wakulima wa zao hili la muhogo katika Wilayah ii ya mkuranga tumefarijika sana kwa ujio wa mradi w akiwanda hiki ambacho kimejengwa na marafiki zetu wa kutoka nchini chini, na tunashukuru kwa jitihada ambazo zinafanywa na Mkuu wetu wa Mkoa wa Pwani pamoja na Rais wetu Dk. John Pombe Magfuli kwa kuwaleta wawekezaji hawa ambao watatusaidia kuondokana na tatizo la kupata soko la uhakika,”walisema wakulima hao.

Kwa  upande wake Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo amewataka maafisa kilimo wote kuhakikisha wanatimiza wajibu wao ipasavyo kwa kuwasimamia vema wakulima wa zao hilo la muhogo  kutonyonywa na walanguzi na  kupata haki zao stahiki na kuahidi kuwaondoa kazini wale wote ambao watabainika kukwamisha juhudi za serikali  katika uwekezaji sekta ya  viwanda.

Aidha Ndikilo alisema kuwa lengo kubwa la serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha inawasaidia kwa hali na mali wananchi wake katika kuondokana na changamoto mbali mbali ambazo zinawakabili ikiwemo ukosefu wa masoko ya ukakiha, ajaira hivyo aatahakikisha zao hilo la muhogo linapata soko kupitia viwanda ambavyo vinajengwa na waekezaji katika maeneo mbali mbali na kuwahimiza wasikate tama na badala yake waendelee zaidi kulima mazao ya biashar ikiwemo ufuta,muhogo na korosho.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Filberto  Sanga amesema kuwa  kipindi cha nyuma wakulima wengine walikuwa tayari  wameshakata tamaa  katika kilimo  cha zao la muhogo,hivyo kumamilika kwa kiwanda hicho kitaweza kuleta mabadili chanya kwa kuwapa fursa wananchi kuwa na soko la uhakika .

“Kwa kweli wananchi wangu hasa kwa wakulima wa zao hili la muhogo katika Wilaya ya Mkuranga baadhi yao walikuwa tayari wameanza kukata tama kabisa na kujikitza zaidi na kilimo cha zo la muhogo nah ii hali ni kutokana na mfumo ambao ulikuwepo wanauza mazao yao kwa bei ya hasara kweli lakini kwa sasa kiwanda hiki kinakamilika mwaka huu hivyo wataondokana kabisa na changamoto ya soko,”alismema Sanga.

Awali akisoma Risala ya ujenzi wa mradi huo  mmoja wa vongozi  wa kiwanda  Leonard Jambeli  kwa niaba ya Mkurugenzi amebainisha kwamba waanategemea kutoa fursa za ajira za moja kwa moja  kwa wazawa zaidi ya mia moja pindi uzalishaji utakapoanza kufanyika rasmi.

KUKAMILIKA kwa mradi huo wa ujenzi wa kiwanda mwishoni mwa mwaka huu  kutaweza kuwa ni mkombozi mkubwa kwa wakulima wa zao hilo katika halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani  ambao kwa miaka mingi walikuwa wanapata hasara kutokana na kunyonywa na walanguzi  kununua zao hilo  kwa bei ndogo.