Home Mchanganyiko MEYA MWITA : NITASHIRIKIANA NA NAIBU ATAKAYECHAGULIWA.

MEYA MWITA : NITASHIRIKIANA NA NAIBU ATAKAYECHAGULIWA.

0

*************

MSTAHIKI Meya wa jiji la Dar es salaam Isaya Mwita amesema kuwa yupotayari kufanya kazi na Naibu Meya yeyote atakayechaguliwa keshokutwa (kesho).

Meya Mwita alitoa kauli hiyo jijini hapa leo (jana) wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa kikao cha robo ya nne ya mwaka cha baraza la madiwani.

Meya Mwita amefafanua kuwa kutokana na wengi kuhama kwenye nafasi zao na kuhamia Chama Cha Mapinduzi CCM, na kwamba bila kujali itikadi ya chama atafanyakazi kwakuwa lengo ni kutumikia wananchi.

“ Uchaguzi wa jiji huwa na mambo mengi, mifano ipo wazi waandishi wa habari huwa mnaona, lakini haimanishi kwamba tutashindwa kufanyakazi kama viongozi ambao tumechaguliwa.

Nitampa ushirikiano mkubwa ambaye atakuwa ameshinda kwenye nafasi hiyo, wote niviongozi, tupo kwa lengo la kuwatumikia wananchi, inapofikia kwenye hatua hii lazima tofauti zetu za kichama tuziweke pembeni” ameongeza Meya Mwita.

Uchaguzi wa Naibu Meya wa jiji hufanyika kila baada ya mwaka mmoja ambapo ,mwakajana idadi ya kura zililingana hivyo kufanya jiji kuongozwa na manaibu wawili kutoka Chama Cha Mapinduzi CCM na Mwingine kutoka Chama Cha Wananchi CUF.

Katika hatua nyingine  madiwani wa jiji hilo wamepitisha taarifa mbalimbali za  maendeleo ikiwa ni pamoja na utendaji wa kamati za jijini hapa.