Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Tiba kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Timothy Wonanji (katikati) akizungumza na baadhi ya viongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila mara baada ya kutembelea hospitalini hapo.
Mhandisi wa Hospitali ya Mloganzila, Happymark John (wa kwanza kushoto) akielezea jinsi tanki la kuhifadhi maji linavyofanya kazi.
Mhandisi Akaniwa Msengi (wa kwanza kushoto) akifafanua jambo kuhusu mtambo wa liquid oxygen.
Mhandisi Msengi akiwaelezea wataalam wa Hospitali ya Mnazi mmoja Zanzibar jinsi mtambo wa oxygen mbadala unavyofanya kazi. Ujumbe wa wataalam hao umetembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila ili kujifunza matumizi ya oxygen kwa wagonjwa.
……………………….
Dar es salaam
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto imesema itaendelea kushirikiana na Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila katika kuhakikisha inatatua changamoto zilizopo ili kuendelea kuboresha utoaji wa huduma za fya.
Kauli hiyo nimetolewa na Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Tiba kutoka Wizara ya Afya Dkt. Timothy Wonanji mara baada ya kutembelea Hospitali ya Mloganzila ili kuangalia utoaji wa huduma, miundominu na changamoto zilizopo.
“Nawapongeza kwa utendaji wenu wa kazi nahidi tutaendelea kushirikiana katika kuhakikisha Hospitali ya Mloganzila inafikia malengo yake na wananchi wanaendelea kupata huduma bora’’amesema Dkt. Wonanji.
Katika hatua nyingine, Ujumbe wa wataalam kutoka Hospitali ya Mnazi mmoja Zanzibar umetembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila ili kujifunza matumizi ya oxygen kwa wagonjwa.
Mkurugenzi wa Uuguzi Hospitali ya Mnazi mmoja Zanzibar, Haji Nyonje Tandu amesema ujumbe huo umehusisha viongozi wa ngazi mbalimbali kwa lengo kujifunza jinsi oxygen inavyopatikana, matumizi yake kwa wagonjwa na kuona namna mitambo inavyozalisha na kusambaza.
“Tumekuja kujifunza kwenu ili tuendelee kuboresha utoaji huduma za afya kwa wananchi kwani hospitali yetu ina matumizi makubwa ya oxygen ikiwa ni wastani wa mitungi 45 kwa siku, hivyo inatupasa kuendelea kujifunza zaidi’’amesema Bw. Haji Nyonje Tandu.