***********
MTAYARISHAJI wa Musiki wa kizazi kipya na mchekeshaji hapa nchini, Rahim Mataja maalufu Cat P, ametangaza kifo cha mama yake mzazi ambacho kimetokea usiku wa kuamkia leo Nyumbani kwao Ubungo Msewe Jijini Dar es Salaam.
Inaelezwa kuwa mazishi yatafanyika kesho katika makaburi ya Rombo Ubungo Jijini Dar es Salaam na msiba upo kwao Ubungo Msewe.
Wengi walikuwa wanamfahamu mama huyo kupitia Tatoo iliyochorwa kwenye mkono wa Cat P hasa kwa kuonesha mapenzi yaliyopo kwa mama yake mzazi.