Waziri wa Nishati Dk. Medard Kalemani akiangalia maji yanyovutwa kwa umeme kutoka katika moja ya shimo la mgodi wa Mkwamba mara baada ya kuwasha umeme katika mgodi huo
Waziri wa Nisahati Dk. Medard Kalemani akizungumza na wachimbaji wa madini baada ya kuwasha umeme katika mgodi wa Mkwamba
Mkuu wa kituo cha Polisi Mlele akiwachukua wakandarasi wa kampuni ya CRCEG baada ya amri ya kukamatwa kwao iliyotolewa na Waziri wa Nishati Dk. Medard Kalemani.
………………………………………………………
Wakandarasi wa mradi wa usambazaji wa umeme vijijini awamu ya tatu mzunguko wa kwanza mkoani katavi; kutoka kampuni ya CRCEG wamekamwatwa kwa amri ya waziri wa nishati Dk. Medard Kalemani baada ya kushindwa kuwasha umeme kwa wakati
Dk. Kalemani ametoa agizo hilo katika kata ya Maji Moto katika halmashauri ya Mpimbwe baada ya kukuta nguzo za umeme zikiwa zimerundikwa katika maeneo kadhaa
Dk Kalemani ametoa agizo hilo baada ya kutoridhishwa na utendaji wa wakandarasi hao kufuatia kuwasha umeme katika vijiji sita kati ya 117 vinavyopaswa kuwashwa umeme
Mradi huo unaogharimu zaidi ya shilingi bilioni 30 unatarajiwa kukamilika desemba mwaka huu huku ukiwa umetekelezwa kwa asilimia 5.1% tu
Waliokamatwa ni pamoja na Mkurugenzi wa Mradi Mhandisi Han Johnny mwenye asili ya kichina na Msimamizi Msaidizi wa mradi huo Mhandisi Arnold Nzali
Akionyesha kukasirika Dk Kalemani aliuliza kushindwa kuwashwa umeme katika kata ya maji ambayo ipo kilomita 27 tu kutoka katika maungio ya mradi huo ambapo hakupata majibu ya kuridhisha
Aidha kurundikwa kwa nguzo katika maeneo kadhaa huku kukiwa hakuna dalili ya vibarua wanaoendelea na kazi
Amesisitiza TANESCO kusimamia kwa karibu ili kuhakikisha mradi unajengwa kwa ubora unaohitajika ili wananchi wapate huduma bora
Katika tukio lingine Waziri huyo wa Nishati aliwasha umeme katika vijiji vya Society, Kilida , Ntibili ambavyo ni vijiji vinavyotekelezwa katika mradi wa kusambaza umeme vijijini
Pia amewasha umeme katika mgodi wa Mkwamba uliopo katika kijiji cha Society uliojengwa na TANESCO kwa gharama ya shilingi bilioni 143