Home Siasa NEC Yamteua Anna Kajigili kuwa Diwani Viti Maalum Chadema

NEC Yamteua Anna Kajigili kuwa Diwani Viti Maalum Chadema

0

Kwa mujibu wa Kifungu cha 86A (8) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika kikao chake cha tarehe 23 Agosti, 2019 imemteua Ndg. ANNA ALINANINE KAJIGILI kuwa Diwani wa Wanawake wa Viti Maalum katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo. 

Uteuzi huu umefanyika baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa, ambaye kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 13(1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, alitaarifu Tume ya Taifa ya Uchaguzi uwepo wa nafasi hiyo wazi ya Diwani wa wanawake wa Viti Maalum, kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) baada ya aliyeteuliwa awali kujiuzulu uanachama wa CHADEMA.