Home Mchanganyiko KAMPENI YA KUTOKOMEZA UGONJWA WA VIKOPE YAZINDULIWA MKOANI PWANI

KAMPENI YA KUTOKOMEZA UGONJWA WA VIKOPE YAZINDULIWA MKOANI PWANI

0
NA MWAMVUA MWINYI,MKURANGA
Mkoa wa Pwani ni miongoni mwa mikoa nchini, yenye idadi kubwa ya wagonjwa wenye vikope(Trachoma) huku wilaya inayoongoza ikiwa ni Mkuranga yenye wagonjwa hao 1,041,wilaya ya Rufiji 191,Kisarawe 243 na Kibiti 207. 
Hayo yalibainika katika kampeni ya kutokomeza ugonjwa wa vikope iliyozinduliwa wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani.

Mkuu wa mkoa huo, mhandisi Evarist Ndikilo  akiwa ni mgeni rasmi katika uzinduzi huo aliiasa jamii kuachana na imani potofu na badala yake wajitokeze kupima ugonjwa huo ili kuweza kupatiwa matibabu na kuondokana na upofu .
Aidha, alitoa rai kwa viongozi  wa kijamii  kuwapeleka wagonjwa wenye vikope katika kambi za uchunguzi ili  kupatiwa matibabu.
Nae meneja mradi wa IMA WORLD HEALTH, Alex Msumanje akielezea magonjwa yasiyopewa kipaombele aliyataja kuwa ni matende,mabusha,minyoo ya tumbo,kichocho,usubi na trachoma(vikope).
Kaimu mratibu wa magonjwa yasiyopewa kipaumbele  wizara ya afya Oscar Kaitaba alisema  watu takribani 11,350 wameshafanyiwa urekebishaji wa kope katika wilaya 21.
Alifafanua, aliwaomba wananchi kujitokeza kufanyiwa urekebishaji wa kope zao kwani huduma hiyo ni bure na mradi huu unafanywa katika mikoa 6 ikiwemo Manyara,Lindi ,Pwani Arusha,Mtwara,na Dodoma.
Kampeni hiyo katika mkoa wa Pwani itafanyika kwenye wilaya nne ikiwa ni pamoja na Kibiti,Kisarawe,Mkuranga na Rufiji.