Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jinsia kutoka Wazara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Julius Mbilinyi (katikati) akizungumza na vyombo vya habari leo Jijini Dar es Salaam kuhusu Kampeni ya Kitaifa ya Kupinga Ukatili wa Kijinsia itakayozinduliwa kesho katika wilaya ya Kigamboni, kulia ni Msanii wa muziki wa kizazi kipya Nurdin Bilal maarufu Shetta kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Jinsia Bi. Mboni Mgaza.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Jinsia Bi. Mboni Mgaza akizungumza na vyombo vya habari leo Jijini Dar es Salaam kuhusu jamii kuachana na Mila na tamaduni zisizofaa zinazochangia kuwepo kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia katika mkutano huo uliolenga kuhabarisha umma kuhusu Kampeni ya Kitaifa ya Kupinga Ukatili wa Kijinsia itakayozinduliwa kesho katika wilaya ya Kigamboni,kulia ni Msanii wa muziki wa kizazi kipya Nurdin Bilal maarufu Shetta
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Nurdin Bilal maarufu kwa jina la Shetta akizungumza na vyombo vya habari leo Jijini Dar es Salaam kuhusu ushiriki wa Taasisi yake ya Shetta Against Women Abuse (SAWA) katika Kampeni ya Kitaifa ya Kupinga Ukatili wa Kijinsia itakayozinduliwa kesho katika wilaya ya Kigamboni
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Elias Barnaba akizungumza na vyombo vya habari leo Jijini Dar es salaam kuhusu ushirki wa wasanii katika kuunga mkono Kampeni ya Kitaifa ya Kupinga Ukatili wa Kijinsia itakayozinduliwa kesho katika wilaya ya Kigamboni.
Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
Na Mwandishi Wetu
Kampeni ya Twende Pamoja Ukatili wa Kijinsia Tanzania sasa basi inatarajiwa kuzinduliwa kesho jijini Dar es Salaam katika Wilaya ya Kigamboni inayolenga kushirikisha wanaume na wanawake kwa lengo la kutoa elimu kwa jamii kupitia mbinu anwai.kwa lengo la kuunganisha nguvu pamoja katika kutokomeza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Maendeleo ya Jinsia kutoka Wazara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Julius Mbilinyi wakati wa akizungumza na vyombo vya habari kuhusu uzinduzi wa Kampeni mpya ya Kitaifa ya kupinga vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto ijulikanayo kama Twende Pamoja.
Aidha Bw. Mbilinyi amesisitiza kuwa Tanzania ni nchi mojawapo kati ya nchi zinazoripotiwa kuwa na vitendo vya ukatili wa kijinsia na asilimia 67 ya kesi zinazoripotiwa za ukatili hutokea kwa wanawake na 33 kwa wanaume.
Ameongeza kuwa Serikali imeliona tatizo hilo na kwa kushirikiana na wadau wengine imeandaa kampeni hiyo itakayosaidia kutoa kwa elimu nchini na kubadilisha fikra hasa kwa wanaume na kwa kiasi kikubwa itapunguza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake ikiwemo mimba na ndoa za utotoni.
Bw. Mbilinyi ameongeza kuwa kwa asilimia kubwa umasikini unachangia kutokea kwa vitendo vya kikatili kwa wnawake na watoto ingawa pia hata kwa wenye vipato vikubwa na vya kati wanakabiliwa na vitendo vya kikatili.
Naye Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Jinsia Bi. Mboni Mgaza amesema kuwa tamaduni na mila zenye madhara zimekuwa ni sababu kubwa kwa jamii kuendeleza vitendo vya kikatili kwa kutolea mfano wa mkoa wa Shinyanga katika miaka ya nyuma vitendo vya mauaji ya wazee wenye macho mekundu vilishamiri ikiushishwa na imani za kishirikina.
Kwa upande wake Msanii wa muziki wa kizazi kipya na Mwenyekiti wa Taasisi ya SAWA Bw. Nurdin Bilal (Shetta) amesema kuwa wao wasanii wameguswa na vitendo vya kukatili kuzidi kuongezeka na wameamua kutumia sanaa yao katika kufikisha ujumbe kwa jamii kuachana na vitendo hivyo vya kikatili dhidi ya wanawake na watoto nchini.