Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya linawashikilia watu nane[8] na watoto watatu[3] wote raia wa nchi ya Burundi wakiwa wameingia nchini bila kibali.
Ni kwamba mnamo tarehe 21/08/2019 majira ya saa 12:30 huko katika Kijiji cha Kasumulu Kata ya Ngana,Tarafa ya Unyakyusa,Wilaya ya Kyela na Mkoa wa Mbeya, askari Polisi wakiwa doria waliwakama watu wazima nane[8] [Umri zaidi ya miaka 20] na watoto watatu [nchini ya miaka 10] wote raia wa nchi ya Burundi wakiwa wameingia nchini bila kibali. Wahamiaji hao haramu walikuwa wakielekea nchini Malawi. Matuhumiwa wote [11] wamekabidhiwa Idara ya Uhamiaji kwa taratibu za kisheria.
TAARIFA YA KUPATIKANA NA BHANGI.
Mnano tarehe 21/08/2019 majira ya saa 20:30 usiku, huko Mwambene kata ya Ilomba, Tarafa ya Iyunga jijini Mbeya. Jeshi la Polisi lilifanikiwa kumkamata JONIOR S/O MBILINYI ,[22] mkazi wa Ilomba ,akiwa na wenzake kumi na tano [15] wakiwa na bhangi gramu [940]. Mbinu iliyotumika ni kujifungia ndani ya chumba nyumbani kwa JUNIOR S/O MBILINYI na kutumia bhangi hiyo. Watuhumiwa watafikishwa Mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.
TAARIFA YA KUPATIKANA NA BHANGI.
Mnamo tarehe 21/08/2019 majira ya saa 10:00 asubuhi huko maeneo ya Uyole –Chemchem, kata ya Igawilo, Tarafa ya Iyunga Jijini Mbeya. Askari Polisi wakiwa doria walimkama ADELA D/O JOHNSON,[25],muhudumu wa bar, na mkazi wa Chemchem akiwa na na bhangi gramu 100. Mtuhumiwa ni muuzaji na mtumiaji wa bhangi hiyo.
Aidha Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea na misako na operesheni mbalimbali katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mbeya ili kuzuia na kudhibiti matukio ya uhalifu pamoja na ajali za barabarani.