Home Mchanganyiko CHUPA 51819 ZAIDI ZA DAMU SALAMA ZAKUSANYWA KWA MWAKA 2018/2019

CHUPA 51819 ZAIDI ZA DAMU SALAMA ZAKUSANYWA KWA MWAKA 2018/2019

0

Meneja Mpango wa Taifa wa Damu Salama Dkt. Magdalena Lyimo akiwasilisha mada ya hali ya upatikanaji wa damu salama nchini kwenye kikao.kazi cha waganga wakuu wa mikoa na halmashauri unaondelea jijini Dodoma.

Mkurugenzi Idara ya TIba kutoka Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe akiongea kwenye kikao.kazi hicho.

Washiriki wa kikao hicho wakifuatilia uwasilishaji wa mada unaoendelea kwenye ukumbi wa CCM

……………………

Na. Catherine Sungura,WAMJW-Dodoma

Mpango wa damu salama umefanikiwa kukusanya chupa 51819 sawa na asilimia ishirini zaidi ya malengo waliyojiwekea kwa mwaka 2018/2019.

Hayo yameelezwa leo na meneja mpango wa taifa wa damu salama Dkt. Magdalena Lyimo wakati akiwasilisha mada ya upatikanaji wa damu kwenye kikao kazi cha waganga wakuu wa mikoa na halmashauri kinachoendelea jijini hapa.

Dkt. Lyimo amesema kwamba kwa mwaka 2018/2019
wizara ya afya kupitia mpango huo uliweka malengo ya kukusanya kiasi cha chupa 309376 nchi nzima ikilinganishwa na chupa 257557 zilizokusanywa mwaka 2017/2018.

Hata hivyo Dkt. Lyimo alisema kuwa wameweza kukusanya chupa 309,376 sawa na,asilimia sitini ya mahitaji ya nchi kulingana na idadi ya wananchi waliopo “tumeweza kufanikiwa kuvuka lengo la kukusanya chupa za damu zaidi na hii ni kutokana na uelewa mkubwa wa wananchi wa kuelewa umuhimu wa kuchangia damu katika kuokoa maisha hususani akina mama wajawazito na wahitaji wengine wa damu”.Alisema.

Aidha, Dkt. Lyimo alitaja makundi ya wachangia damu kuwa wanawake ni asilimia 14 pekee huku idadi ya wanaume ikiwa ni asilimia 86 hapa nchini.

Hata hivyo alisema hali ya maambukizi ya magonjwa kwa damu zinazobainika katika ukusanyaji huo ameeleza kuwa ugonjwa wa homa ya Ini ndio inayoongoza kwa asilimia 5.9 ikifuatiwa HIV kwa asilimia 2.8.

Dkt. Lyimo amewashukuru wananchi wanaoendelea kuchangia damu ikiwemo vijana watumishi wa umma, taasisi na mashirika mbalimbali kwa moyo wa kutekeleza zoezi hilo ili kufikia malengo yanayotarajiwa.