Baadhi ya wakazi wa kata ya Kakese wakiwa katika mkutano wa uzinduzi wa mfuko wa CHF iliyoboreshwa
Aliyekaa katikati ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Mpanda Sostenes Mayoka, kushoto kwake ni Naibu Meya Lucas Kanoni na kulia kwake ni Afisa Utumishi wa Manispaa Deodatus Kangu.
************
Na Mwandishi wetu, Katavi
WAKAZI WA KAKESE WAMESHINDWA KUJIANDIKISHA KWENYE MFUKO AFYA YA JAMII
Wakazi wa kata ya Kakese katika Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wameshindwa kujiandikisha katika mfuko wa afya ya jamii (CHF iliyobororeshwa) tangu kuanza kwa uandikishaji wa mfuko huo mwezi juni mwaka huu
Ni kaya mbili tu kati ya kaya 2,577 za kata hiyo zilizojiandikisha; hali inayopelekea wakazi hao kuendelea kutumia fedha kutibiwa katika hospitali za watu binafsi ambapo kata hiyo ina jumla ya vijiji vinne na vitongoji 18
Wakazi wa kata hiyo walipozungumza na mwandishi wa habari wamedai kuwa walikuwa na hofu ya kujiandikisha kutokana na tatizo la kutopatikana dawa katika zahanati yao mara kwa mara
Akizungumza katika mkutano wa uzinduzi wa mfuko huo mratibu wa mfuko wa CHF iliyoboreshwa mkoa wa katavi bwana Bahati Mwailafu amewataka wakazi hao kubadilika na kujiunga na mfuko ambao ameutaka kuwa mkombozi katika afya ya familia
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Mpanda; Katibu Tawala wa Wilaya hiyo bwana Sostenes Mayoka amesema uandikishaji katika Manispaa ya Mpanda umezorota tofauti na Halmashauri nyingine za mkoa wa Katavi
Aliongeza kuwa jumla ya kaya 89 zenye wanufaika 358; kati ya kaya zaidi ya 8,000 za wilaya ya Mpanda ndizo zimejiunga na mfuko huo
Akizungumzia hali ya kutokujitokezakwa wananchi kujiunga na mfuko huo diwani wa kata ya Kakese bwana Maganga Salaganda amesema wananchi walikuwa hawajapata elimu ya kutosha juu ya mfuko huo ndio sababu wakakosa imani nao
Bwana Salaganda aliongeza kuwa anategemea wananchi watajitokeza mara baada ya mkutano huo kumalizika nap engine itakuwa kata itakayoongoza katika uandikishaji wanachama wa mfuko wa afya ya jamii