Home Burudani FAINALI ZA MISS TANZANIA KUFANYIKA AGOSTI 23, 2019 MILLENIUM TOWER MAKUMBUSHO

FAINALI ZA MISS TANZANIA KUFANYIKA AGOSTI 23, 2019 MILLENIUM TOWER MAKUMBUSHO

0

Mkurugenzi wa Kampuni ya The Look inayoandaa Fainali za Mashindano ya urembo ya Miss Tanzania 2019 akizungumza na waandishi wa habari katika hoteli ya Serene iliyoko Mbezi Beachi jijini Dar es salaam leo.

Washiriki wa shindano la Miss Tanzania 2019 wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya mkutano na waandishi wa habari katika hoteli ya Serene Mbezi Beach jijini Dar es salaam leo.

……………………………………………….

Fainali za Mashindano ya urembo ya Miss Tanzania 2019 chini ya uongozi mpya wa Kampuni ya The Look ambayo yalianza mapema mwezi April 2019 yatafikia kilele chake tarehe 23 Agosti 2019 katika Ukumbi wa New Millennium Towers LAPF uliopo eneo la Makumbusho jijini D’salaam.

Washiriki wapatao 20 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania tayari wapo kambini tangu tarehe 12 Agosti 2019 wakijiandaa na kinyang’anyiro hicho cha kuwania taji hilo.

Kufanyika kwa Fainali hizi ni hitimisho ya mashindano ya mikoa .na kanda ambayo yalifanyika katika kipindi cha kuanzia mwezi April hadi Julai 2019. 

Wakiwa kambini Warembo hawa wameshiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii, ikiwa ni pamoja na kutembelea katika Kituo cha Watoto wetu Tanzania kilichopo eneo la Mbezi Mwisho jijini D’salaam Kituo ambacho kinatunza watoto wanaoishi katika Mazingira magumu.

Wakiwa katika Kituo hicho warembo wetu wameweza kuwafariji watoto hao kwa kucheza nao Michezo ya aina mbalimbali na kula nao pamoja.

Warembo pia wameshiriki katika mashindano madogo yajulikanayo kama Fast Tract na kuweza kufanya vizuri katika mashindano hayo ya kumtafuta

  1. Mrembo mwenye kipaji – Miss Talent
  2. Mrembo mwenye mvuto katika picha – Miss Photogenic
  3. Mrembo mwanamitindo – Top Model
  4. Mrembo mwanamichezo – Top sports woman
  5. Mrembo chaguo la watu – Miss Personalit

Warembo hao wapo ambao wameingia katika hatua ya Tano Bora na washindi katika mashindano hayo watatangazwa katika Fainali usiku wa tarehe 23 Agosti 2019.

Maandalizi yote yameshakamilika kinachosubiriwa kwa hamu ni tukio lenyewe.