Home Michezo SIMBA NA YANGA VETERANS USO KWA USO  AGOSTI 17 MTWARA KWENYE TAMASHA...

SIMBA NA YANGA VETERANS USO KWA USO  AGOSTI 17 MTWARA KWENYE TAMASHA LA MTAA KWA MTAA

0

Na Asha Said, DAR ES SALAAM
WACHEZAJI wa zamani wa Simba na Yanga wanatarajiwa kumenyana katika kandanda safi la hitimisho la tamasha la mtaa kwa mtaa linalotarajiwa kutimua vumbi katika Uwanja wa Ilulu Mkoani Lindi.
Tamasha hilo la aina yake linatarajia kuwakutanisha wakongwe hao wa kukinukisha, Agost 17 kabla ya AgostI 18 kupigwa fainali ya tamasha hilo iliyozishirikisha timu zaidi ya 100.
Akizungumza mjini Dar es Salaam jana, Mkuu wa Masoko wa Kampuni ya Mashujaa, Maximilian Luhanga,  amesema  katika hitimisho la tamasha lao liloanza mwaka jana, wameamua kuwahita wakongwe hao wa soka ili kunogesha tamasha lao.

Amesema, siku ya hitimisho timu mbili zitamenyana katika mchezo huo wa fainali ambapo bingwa atazawadiwa gari aina ya Noah ambayo kwa imani yao itawasaidia katika kujiongezea kipato au timu kuitumia katika safari zao mbalimbali.
“Tumeona tutoe zawadi ya gari kwa maana itawasaidia katika mambo mbalimbali tofauti na zawadi ya pesa zinatumikazinaisha lakini gari litawasaidia katika mambo mengi,”amesema                              Kwa upande wa wachezaji Thomas Kipese ‘Uncle’
ambaye ni mchezaji wa Simba, aliwataka vijana kujitokeza kwa wingi siku hiyo ili waweze kupata vitu vizuri kutoka kwao.
Amesema, na katika mchezo huo Yanga lazima wafe kama walivyokufa Songea katika Tamasha la Majimaji, na kukiri kuwa kikosi chao kimejipanga vya kutosha kwa ajili ya mchezo huo.
“Mimi mnanijua vizuri wadaau wa mpira mje kwa wingi sana siku hiyo nmpate burudani ya aina yake, iliyoandaliwa na Mashujaa FM iliyopo Lindi, ni nafasi ya kipekee kwa wakazi wa mkoa huo kujionea burudani ya aina yake,”alisema.
Naye Ramadhan Kampira kwa upande wa wachezaji wa Yanga, aliwataka Simba kujiandaa kisaikolojia kwenda kupokea kipigo kwani Yanga iko vizuri na wanamorali ya hali ya juu kwa ajili ya mchezo huo.
Aliwataja baadhi ya wachezaji watakaolitandaza soka siku hiyo kuwa ni yeye mwenyewe, Mohamed Hussein, Edibily Lunyamila, Bakari Malima, Said Maulid na wengine ambao watakuwepo kwenye kikosi na msafara wao wa kwenda mkoani Lindi.