Home Michezo LIVERPOOL YAICHAPA 5-4 CHELSEA KWA PENALTI NA KUTWAA SUPER CUP YA UEFA

LIVERPOOL YAICHAPA 5-4 CHELSEA KWA PENALTI NA KUTWAA SUPER CUP YA UEFA

0
Kipa Mspaniola, Adrian San Miguel del Castillo akiwa ameshika taji la Super Cup la UEFA katika picha ya pamoja na wachezaji wenzake wa Liverpool baada ya kuiwezesha timu yao kuifunga Chelsea kwa penalti 5-4 kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika 120 usiku wa jana Uwanja Vodafone Arena mjini İstanbul, Uturuki. Mabao ya Chelsea yalifungwa na Olivier Giroud dakika ya 36 na Jorginho dakika ya 101 kwa penalti, wakati ya Livepool yote yalifungwa na Sadio Mane dakika ya 48 na 95 kabla ya Adrian kupangua mkwaju wa penalti wa Tammy Abraham.
Waliofunga penalti za Liverpool ni Roberto Firmino, Fabinho, Divock Origi, Trent Alexander-Arnold na Mohamed Salah wakati za Chelsea zilifungwa na Jorginho, Ross Barkley, Mount na Emerson PICHA ZAIDI SOMA HAPA