Home Mchanganyiko DC ASSUMPTER AIPONGEZA OSHA KWA KUSIMAMIA UTEKELEZAJI WA SHERIA YA USALAMA WA...

DC ASSUMPTER AIPONGEZA OSHA KWA KUSIMAMIA UTEKELEZAJI WA SHERIA YA USALAMA WA AFYA

0

***************

Mkuu wa Wilaya Kibaha Mh Assumpter N. Mshama ameipongeza OSHA kwa
kusimamia utekelezaji wa sheria ya Usalama na Afya Mahali pa kazi nchini kwa
kufika sehemu kubwa wilaya humo,

Akizungumza mara baada ya kutembelea Ofisi za OSHA jijini Dar es salaam, Mh.Assumpter amesema amemua kutembelea ofisi za OSHA kutoa pongezi kwa ushirikiano mkubwa walioupatia Wilaya hiyo kutokana zoezi la ukaguzi wa Viwanda ambalo OSHA ilifanya, kwa kukagua maeneo ya kazi hususani Viwanda vilivyopo Wilayani Kibaha kuona utekelezaji wa sheria ya usalama na Afya mahali pa kazi.

Aidha Mkuu huyo wa wilaya, amewataka wamiliki wa Viwanda Wilayani Kibaha
kuhakikisha wanazingatia sheria ya usalama na Afya Mahali pa Kazi, ili kulinda
nguvu kazi, na kuunga mkono Juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dr. John Pombe Magufuli, katika ujenzi wa Viwanda.

Mshama ameongeza kuwa Katika kuunga juhudi hizo za Mh. Rais ambapo pia nchi
za SADDC zimemuunga mkono Mh Rais John Pombe Magufuli, katika zima za
ujenzi wa Viwanda nchini, amesema sisi lazima tuendeleze juhudi hizo ili tuweze
kufikia malengo hayo ambayo Mh. Rais anataka kufikia.

Naye Kaimu Mtendaji Mkuu wa OSHA Bi Khadija Mwenda, amesema wataendelea
kusimamia sheria ya usalama na Afya kama sheria inavyoelekeza ili kuweza
kulinda wafanyakazi katika maeneo ya kazi.

Bi.Khadija amemshukuru mkuu huyo wa wilaya kuja kutembelea Ofisi za OSHA na kuwapa mrejesho juu ya zoezi maalamu la Ukagauzi lilofanywa na OSHA kwa lengo la kukagua maeneo ya kazi wilaya Kibaha kuona utekelezaji wa sheria ya usalama na Afya, kutokana na Wilaya hiyo kuwa na Viwanda Vingi hapa nchini.