Home Mchanganyiko WAKAZI WA PANDE NA MLINGOTINI WASEMA CHONDE CHONDE WAONANE USO KWA USO...

WAKAZI WA PANDE NA MLINGOTINI WASEMA CHONDE CHONDE WAONANE USO KWA USO NA RAIS.DK.MAGUFULI KUJUA HATMA YA FIDIA ZAO

0
NA MWAMVUA MWINYI,BAGAMOYO
WAKAZI wa kijiji cha Pande na Mlingotini ,Bagamoyo mkoani Pwani ambao walitakiwa kuhama kupisha mradi wa bandari mpya ya Bagamoyo wamemuangukia Rais dk.John Magufuli aone umuhimu wa kwenda kutoa kauli yake ya mwisho,kuhusu hatma ya fidia zao na eneo wanalopaswa kuhamia.
Wamedai ni zaidi ya miaka saba tangu wafanyiwe tathmini na kuahidiwa watahamishwa eneo jingine lakini imekuwa ni hadithi inayowaacha katika sintofahamu.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti ,juu ya suala hilo wakati mbunge wa jimbo la Bagamoyo, alhaj dk.Shukuru Kawambwa alipofanya ziara yake ya jimbo na kupeleka mrejesho wa kusitishwa kwa ujenzi wa Bandari kavu kwa sasa ,walimueleza wanamtaka Rais na sio mtu mwingine.
Wakazi akiwemo mzee Rajabu Wading’ola na Matata alisema ,serikali ione uchungu ,iangalie nafsi zao zinavyohangaika kwa muda mrefu .
“Ni kama tumesuswa ,hatuna msaada ,eneo hili lilishajengwa shule watoto wetu wanasoma ,kuna msikiti,zahanati, “alieleza Wading’ola.
“Baadhi ya watu walilipwa fidia lakini wengine hawajalipwa huku wengine wakiwa wamepunjwa fidia zao kwa kulipwa kidogo fedha ambazo hazitoshi kununulia maeneo mengine” Matata alisema.
Aidha alitaja changamoto nyingine ni ufugaji holela wa ng’ombe unaofanywa na wamang’ati ambapo mifugo hiyo imekuwa ikila mazao yao huku kukiwa hakuna msaada wowote kisheria.
Kwa upande wake mbunge wa Jimbo la Bagamoyo Dk Shukuru Kawambwa alipokea agizo na malalamiko hayo kutoka kwa wananchi na kudai atalishughulikia kuhakikisha anafanikiwa.
Aliwaambia, serikali imesitisha ujenzi wa Bandari kavu Bagamoyo baada ya kubaini mwekezaji kuweka masharti magumu ya kimkataba na kuonekana kubana maslahi ya watanzania na nchi kijumla.
“Serikali isingeweza kukubali masharti yanayobana uchumi wetu,haiwezekani baada ya ujenzi huo ,Tanzania kutoruhusiwa kujenga na kuendeleza bandari nyingine kuanzia Tanga mpaka Mtwara na pia kushindwa kukusanya kodi katika bandari hiyo, “:-kutokana na masharti hayo serikali isingeweza kukaa kimya “,serikali inajua changamoto mliyonayo na inafanyia kazi”       
Kawambwa alifafanua, kijiji cha Pande kina kaya 2,200 sawa na watu 16,500 ambao walitakiwa kuhama eneo hilo.
Alisema, jambo hilo limekuwa ni changamoto kubwa ,wananchi hawamuelewi hivyo kuna haja ya suala hilo kufikia mwisho.