Home Mchanganyiko RC NDIKILO AANZA ZIARA YA VIWANDA 14 AMBAPO 13 ATAWEKA JIWE LA...

RC NDIKILO AANZA ZIARA YA VIWANDA 14 AMBAPO 13 ATAWEKA JIWE LA MSINGI NA KIMOJA ATAKIKAGUA

0

**********

NA MWAMVUA MWINYI,PWANI
MKUU wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo ameanza ziara ya kutembelea viwanda 14 ikiwa ni sehemu ya viwanda 1,192 vilivyojengwa mkoani humo.
Katika ziara hiyo, mkuu huyo wa mkoa ataweka mawe ya msingi katika viwanda 13 na kimoja atakikagua ujenzi wake.
Hayo yalisemwa mjini Kibaha na Katibu Tawala wa mkoa (RAS) Pwani Theresia Mbando alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya ziara ya kikazi itakayofanywa na mkuu wa mkoa huo.
“Jumla ya viwanda vilivyojengwa kati ya hivyo vikubwa ni 56, vya kati 85, vidogo ni 350 na vidogo sana ni 701 vikiwa vimejengwa kwenye wilaya za mkoa huu”.
Akizungumzia juu ya Ziara hiyo anasema kuwa ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Magufuli la ujenzi wa viwanda ili kuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo 2025.
Alisema, viwanda hivyo viko kwenye hatua mbalimbali za ujenzi huku vingine vikiwa vimeanza uzalishaji ambavyo ni Lake Steel, Shafa Investment na Super Meals.