Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), Stergomena Tax akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa Machapisho matano ya Kituo cha Utafiti na Machapisho cha Jumuiya hiyo kwenye ukumbi wa Julius Nyerere leo jijini Dar es salaam.
Madaraka Nyerere Mwana wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere na Mjumbe wa bodi ya Kituo cha Utafiti na Machapisho cha Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari katika uzinduzi huo.
Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), Stergomena Tax akiwa pamoja na viongozi wengine wakizindua Machapisho cha Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) kutoka kulia ni Waziri wa Nishati Dk. Merdad Kalemani, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu na kutoka kushoto ni Madaraka Nyerere Mwana wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere na Mjumbe wa bodi ya Kituo cha Utafiti na Machapisho cha Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) na Bw. Munetsi Mdakufamba Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Utafiti na Machapisho cha Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC)
Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), Stergomena Tax akipongezana na viongozi wengine baada ya kizindua Machapisho cha Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) kutoka kulia ni Waziri wa Nishati Dk. Merdad Kalemani, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu na kutoka kushoto ni Madaraka Nyerere Mwana wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere na Mjumbe wa bodi ya Kituo cha Utafiti na Machapisho cha Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) na Bw. Munetsi Mdakufamba Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Utafiti na Machapisho cha Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC)
Waziri wa Nishati Dk. Merdad Kalemani akizungumza katika uzinduzi huo.
Picha ya Pamoja.
(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWEBLOG)
………………………………………………
NA JOHN BUKUKU
Tanzania inahitaji kuongeza juhudi ili kufikia malengo ya uwezeshaji wa wanawake katika masuala ya uchumi na siasa, kuendana na malengo ya mkakati wa Maendeleo ya Jinsia wa mwaka 2018.
Akizungumza katika uzinduzi wa machapisho matano ya Kituo cha Utafiti na Machapisho cha Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SARDC), Katibu Mtendaji wa SADC, Stergomena Tax amesema japokuwa Tanzania inajitahidi katika kufikia malengo yaliyowekwa bado kunatakiwa juhudi zaidi ili kufikia malengo.
Amesema katika chapisho la Tathmini ya Maendeleo ya Jinsia ya mwaka 2018, inaonyesha kuwa katika nchi wanachama wa SADC ni nchi mbili zilizofikia malengo ya kuwa na asilimia 50/50 bungeni, ambazo ni Afrika Kusini na Seychelles.
“Tanzania inafanya vizuri ikilinganishwa na nchi nyingine, lakini tunahitaji juhudi zaidi ili kufikia malengo haya na mengine mengi yaliyowekwa kupitia jumuiya hii,” amesema.
Dk Tax alisema katika chapisho la kwanza lililozinduliwa jana linaloeleza kuhusu mkakati wa maendeleo wa SADC hasa katika mkakati wa kuwajumuisha wanawake katika masuala ya Ulinzi na Usalama wa mwaka 2018-22, unaonesha kuwa suala hilo ni muhimu hasa kwa kuwa usalama unapoyumba wanaoumia zaidi ni wanawake na watoto.
Amesema katika chapisho la nne, linaloelezea mkakati wa mpango wa kushughulikia matatizo ya kijinsia hali bado siyo nzuri hivyo juhudi zaidi zinahitajika katika kuelimisha umma ili kuhakikisha unyanyasaji huo unapungua kwa kiwango cha juu.
Katika suala la nishati, linaloelezwa katika chapisho la nne, Dk Tax alisema inaonesha kuwa nchi nyingi wanachama bado hazijagusia suala la uzalishaji wa nishati hasa za gesi na mafuta na kuziweka pamoja kwa mamatumizi ya nchi wanachama.
Amesema nchi nyingi wanachama wa SADC, ikiwamo Tanzania zina utajiri mkubwa wa nishati hizo lakini bado hazijafanya jitihada za kuhakikisha mkakati wa pamoja wa uvunaji wa nishati hizo unafanikiwa.
Naye Waziri wa Nishati Mh. Dk.Meldad Kalemani amesema Tanzania imetekeleza kwa kiwango chake miradi inayohusisha SADC na kwa upande mwingine EAC hasa katika njia za kusafirisha umeme.
Hivi sasa katika nchi yetu tunajenga miundombinu ya kusafirisha umeme kwenye kona zote nne ambapo sasa ajenda ni kuzalisha umeme , Kusambaza na kujenga miundimboni ya kusambaza umeme.
Tukishajenga njia za kusafirisha umeme ni wazi tutaweza kuwaunzia wenzetu katika nchi za SADC na EAC ambapo mpaka sasa kuna mradi wa kuziunganisha nchi za ,Tanzania Zambia na Kenya ambao umeshaanza. na huo ni mradi muhimu katika kuunganisha umeme kwa nchi za SADC , Hivyo mradi wa umeme bonde la Rufuji utakapokamilika umeme utauzwa kwa nchi nyingine za SADC kama Malawi , Zambia na Congo DRC.kwenda mpaka Malawi na tayari tumepata fedha kutoka benki ya dunia.
Kona ya kwanza tunajenga njia za kusafirisha umeme wa Megawati 400 kutoka Dar es salaam kwenda Kaskazini , Namanga ambao utakwenda mpaka nchini Kenya.
Kona ya pili ni kuutoa umeme kutoka Iringa Mbeya, Sumbawanga, Kigoma mpaka Nyakanazi na kufafanua unaopita Kigoma mpaka DRC Kongo kwa sababu makubaliano ni kuuziana umeme kulingana na mahitaji.
Hata hivyo amefafanua kukiwa na umeme wa kutosha maana yake maeneo mengi ya vijiji yatakuwa na umeme wa uhakika na hivyo kutaisaidia kupunguza uharibifu wa mazingita utakwenda na kuwaondolea changamoto mbalimbali wanawake ambao ndiyo wenye matumizi makubwa ya kuni na mkaa.