Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk Zainab Chaula akifungua mafunzo ya wakaguzi wa Mifumo ya uzalishaji Dawa na Vifaa tiba (GMP) kwa nchi wanachama wa SADC ambapo Tanzania ndiyo mwenyeji , Wakufunzi wa mafunzo hayo wanatoka Malmaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) katikati ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TMDA Adam Fimbo Mafunzo hayo yanafanyika kwenye hoteli ya Habour View jijini Dar es salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TMDA Adam Fimbo akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya wakaguzi wa Mifumo ya uzalishaji Dawa na Vifaa tiba (GMP) kwa nchi wanachama wa SADC ambapo Tanzania ndiyo mwenyeji Mafunzo hayo yanafanyika kwenye hoteli ya Habour View jijini Dar es salaam.
Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Nchini –TMDA wametoa mafunzo kwa wakaguzi wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika –SADC ili kuondoa changamoto ya uingizwaji wa Dawa feki katika nchini hizo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto, Bi Zainabu Chaula amesema Tanzania imepiga hatua katika suala la usimamizi bora wa Dawa na imetunukiwa cheti cha Mifumo bora ya usimamiaji wa dawa na vifaa na kuwa ya kwanza kwa nchi zote za Afrika.
Awali akielezea mafunzo hayo Bi Zainabu amesema kupitia siku hizo 12, -TMDA itatoa mafunzo kwa washiriki kutoka nchi hizo za SADC ili kudhibiti uingizwaji wa Dawa feki katika mipaka ya nchi zote hizo lakini pia kutumia fursa hiyo ili kuweza kugawana ujuzi wa udhibiti wa dawa pamoja na vifaa tiba.
Pia amesema Dawa nyingi feki zimekuwa zikipita katika mipaka ya nchini hizo hivyo kupitia ushirikiano huo utasaidia kumaliza tatizo hilo na kufanya wananchi kuwa na uhakika wa dawa.
Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa –TMDA, Bw.Adam Fimbo amesema mafunzo hayo yameandaliwa na chini za SADC ili kufundisha watumishi wa nchi hizo kufanya kazi nzuri ili kusaidia udhibiti wa dawa na vifaa tiba katika nchi za SADC
Amesema kupitia mafunzo hayo itasaidia kutengeneza mifumo bora na inayofanana itakayosaidia kudhitibi suala la dawa ambazo hazifai kwa matumizi ya Binadamu, Mafunzo hayo yatadumu kwa siku 11ambapo yalianza tarehe 12 na yatamalizika Agosti 23 mwaka huu.
Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Nchini –TMDA wametoa mafunzo kwa wakaguzi wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika –SADC ili kuondoa changamoto ya uingizwaji wa Dawa feki katika nchini hizo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto, Bi Zainabu Chaula wakati wa hafla ya Ufunguzi wa Mafunzo hayo amesema Tanzania imepiga hatua katika suala la
usimamizi bora wa Dawa na imetunukiwa cheti cha Mifumo bora ya usimamiaji wa dawa na vifaa katika nchini zote za Afrika.
Awali akielezea mafunzo hayo Bi Zainabu amesema kupitia siku hizo 12, -TMDA itatoa mafunzo kwa nchi hizo za SADC ili kudhibiti uingizwaji wa Dawa feki katika mipaka ya nchi zote hizo lakini pia kutumia fursa hiyo ili kuweza kugawana ujuzi wa tiba pamoja na vifaa tiba.
INSERT………CHAULA.
Pia amesema Dawa nyingi feki zimekuwa zikipita katika mipaka ya nchini hizo hivyo kupitia ushirikiano huo ukasaidia kumaliza suala hilo na kufanya wananchi kuwa na uhakika wa dawa.
Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa –TMDA,
ADAM FIMBO amesema mafunzo hayo yameandaliwa chini ya nchini za SADC ili kufundisha watumishi wa nchi hizo kufanya kazi nzuri ili kusaidia wananchi kupata huduma bora.
INSERT……FIMBO.
Amesema kupitia mafunzo hayo itasaidia kutengeneza mifumo bora na inayofanana itakayosaidia kudhitibi suala la dawa ambazo hazifai kwa matumizi ya Binadamu huku Mafunzo hayo yatadumu kwa siku 11ambao yameanza
tarehe 12 na kumalizika Agosti 23 mwaka huu.
Mratibu wa Mradi wa SADC Medicines Reguratory Harmonisation Project (SMRHP) Bi. Sakhile Dube Mwedzi akizungumza katika uzinduzi wa mafunzo hayo.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba TMDA Bi. Gaudensia Simwanza akimkaribisha kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo ili kuzingumza na washiriki wa mafunzo hayo.
Picha mbalimbali zikiwaonesha washiriki wa mafunzo hayo wakiwa wakifuatilia hotuba ya ufunguzi kutoka kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk Zainab Chaula wakati alipokuwa akizungumza.