Mkurugenzi Mkuu wa MSD Laurean Bwanakunu akiwa pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja na Shughuli za Kanda wa MSD Salome Mallamia na Meneja wa MSD Kanda ya Dar es Salaam inayohudumia mkoa wa Morogoro Celestine Haule wakiendelea kupokea dawa zaidi za kukabidhi hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Morogoro kwa ajili ya kuhudumia majeruhi
…………………………………………………
Timu ya MSD ikiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bw. Laurean Bwanakunu wakiwa sambamba na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Mohamed Kambi, wamewatembelea majeruhi wa ajali ya moto, iliyosababishwa na mlipuko wa lori la mafuta waliolazwa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.
Pamoja na kuwajulia hali majeruhi hao, ujumbe huo pia umelenga kufuatilia na kufahamu misaada ya haraka ya kitabibu inayohitajika kwa sasa hospitalini hapo ili kusaidia majeruhi.
Aidha, wajumbe hao, wamewasilisha msaada wa dawa na vifaa tiba kwenye hospitali hiyo.