Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza na Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Mhe. Mubarak Al-Sehaijan kuhusu kupeleka wataalam wa kwenye vituo vipya vya afya vilivyoanzishwa nchini.Wengine kulia ni maofisa kutoka Balozi wa Kuwait na Wizara ya Afya.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akiwa na Balozi Mubarak Al-Sehaijan baada ya kumalizika kwa mazungumzo hayo.
************
Na John Stephen
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu amekutana na Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Mhe. Mubarak Al-Sehaijan na kujadiliana kuhusu kushirikiana kupeleka wataalam wa afya kwenye vituo vipya vya afya vilivyoanzishwa nchini.
Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Mhe. Mubarak Al-Sehaijan amefanya mazungumzo na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu na kukubaliana Kuwait kupeleka wataalam wa afya katika vituo mbalimbali vya afya vilivyojengwa nchini na serikali ya awamu ya tano.
Katika mazungumo hayo Waziri Ummy Mwalimu kwa pamoja wamekubaliana madaktari bingwa wa mishipa ya fahamu na madaktari bingwa wa moyo kuja nchini kwa lengo la kubadilishana uzoefu na wataalam wetu katika maeneo hayo mawili.
“Tumekubaliana na Balozi Mubarak Al-Sehaijan kwamba kutakuwapo na mpango wa kuendelea kupunguza vifo vya mama na mtoto kwa kutumia wataalam wetu na wale wa Kuwait,” amesema Waziri Ummy Mwalimu.
Baada ya majadiliano hayo Waziri Ummy Mwalimu aliagiza kuandaliwa kwa utaratibu wa utekelezaji wa maeneo hayo matatu waliokubaliana ambayo ni; kupeleka wataalam wa afya kwenye vituo vipya vya afya nchini, madaktari bingwa mishipa ya fahamu na moyo kushirikiana na wataalam wetu na kupunguza vifo vya mama na mtoto kwa kushirikiana na wataalam wa Kuwait.