Home Mchanganyiko Kampuni ya Green Mile Safari imekanusha kufutiwa umiliki wa kitalu cha Uwindaji

Kampuni ya Green Mile Safari imekanusha kufutiwa umiliki wa kitalu cha Uwindaji

0

**********

NA EMMANUEL MBATILO

Kampuni ya Green Mile Safari imekanusha taarifa zinazozagaa kwenye mitandao ya kijamii zinazomuhusisha Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt.Hamis Kigwangala kuwa amefuta umiliki wa kitalu cha uwindaji wa kitalii cha Lake Natron East kinachomilikiwa na kampuni hiyo.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam,Mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo Bw.Said Mndeme amesema kuwa taarifa hizo zinazozagaa ni muendelezo wa mkakati wa kuichafua kampuni na kuiharibia biashara yake.

Aidha Bw.Mndeme amesema kuwa wanawajulisha walioguswa na kadhia hiyo kuwa shughuli za uwindaji wa kitalii za kampuni hiyo zitaendelea kama kawaida kwa kufuata sheria,taratibu na kanuni za nchi.

“Tumepata migogoro mingi tokea mwaka 2012 mara baada ya kumilikishwa kitalu hiki na wizara.Kampuni ya Wengert kwa kuwatumia watendaji wachache waliopo katika wizara ya maliasili na Utalii na pia ndani ya halmashauri ya Longido wametusababishia usumbufu mkubwa”.Amesema Bw.Mndeme.

Pamoja na hayo Bw.Mndeme amesema kuwa Wingert Windrose Safari wamewafungulia kesi nyingi kampuni hiyo pamoja na Serikali mwaka 2013 kudai wamilikishwe Kitalu hicho na kesi zote wameshinda na sasa wanataarisha demand note dhidi ya kampuni ya Wengert kuwaharibia biashara na jina lao katika masoko ya kimataifa na nakala zipo na katika madai hayo pia serikali itaweza kurudisha pesa ilizopoteza.

Hata hivyo kwa upande wa taarifa kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii kuhusu malalamiko ya Kampuni ya Friedkin Conservation Fund juu ya umiliki wa kitalu cha Uwindaji(kwa mujibu wa Kampuni ya Green Mile Safari) ilieleza kuwa baada ya matokeo ya ugawaji wa vitalu kampuni zote mbili Tanzania Game Trackers Safaris Ltd (TGTS)pamoja na Wengert Windrose Safaris (WWS)ziliwasilisha rufaa kwa waziri wa maliasili na utalii kupitia kamati ya ushauri wa ugawaji vitalu (iliyokaa Januari 2012) kutaka kufahamu sababu za kutokupewa baadhi ya vitalu walivyoomba kikiwepo cha Lake Natron Game Controlled Area (North).