KIONGOZI wa mbio za mwenge kitaifa 2019,Mzee Mkongea Ali ameridhia na kuukubali uendelevu wa mradi wa ujenzi wa hospital ya magonjwa ya saratani (Good Samaritan) ,kata ya Viwanja Sita ,Ifakara,Morogoro ,ambao unatarajiwa kugharimu sh.bilioni 5 hadi kukamilika kwake.
Fedha hizo ni za wadau na wahisani ambapo mradi huo unatekelezwa kwa kushirikiana na shirika la kimissionary Humma na kanisa katolik jimbo la Ifakara na,utekelezaji wake ulianza desemba 2015.
Mradi unahusisha ujenzi wa hospital ambayo itakuwa ikitoa huduma ya matibabu ya magonjwa ya saratani hususan kwa wananchi wenye kipato cha chini ambao hawawezi kumudu gharama hizo kwenye hospital nyingine nchini na nje ya nchi.
Kutoa huduma ya kutibu magonjwa ya saratani hususan kwa watu wenye kipato cha chini wanaopatikana maeneo ya karibu na halmashauri ya Ifakara na mikoa jirani kama vile Iringa,Ruvuma, Njombe,Mtwara,Lindi,Pwani,Dodoma,Morogoro,Singida na maeneo mengine Tanzania.
Mradi pia unalenga kujenga majengo mbalimbali ya kutolea huduma ikiwa majengo ya wodi,jengo la utawala,jengo la mapokezi,la mkutano,la mionzi,CT scan/MRI ,maabara,chumba cha upasuaji.
Majengo yote yamefikia asilimia 100 isipokuwa jengo la mionzi