Mkurugenzi wa halmashauri ya jiji la Arusha Dkt.Maulid Madeni akitoa baadhi ya ufafanuzi na kuongea kwenye kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri ya jiji la Arusha picha na ahmed mahmoud Arusha
Mstahiki meya wa jiji la Arusha Kalist Lazaro akiwa na mkurugenzi wa halmashauri ya jiji la Arusha Dkt.Maulid Madeni kwenye kikao cha kawaida cha robo ya mwisho katika ukumbi wa shule ya sekondari Arusha picha na ahmed mahmoud Arusha
……………………………………………………….
BARAZA la madiwani wa halashauri ya jiji la Arusha,limemuagiza mganga mkuu wa jiji hilo kuendesha kampeni maalumu ya chanjo ya ugonjwa wa Ini ,ambao ni hatari na hauna dawa pia umekuwa ni tishio kwa maisha ya binadamu .
Agizo hilo limetolewa na Mstahiki wa jiji la Arusha ,Kalisti Lazaro, Augosti 9 kwenye kikao cha baraza hilo kilichofanyika kwenye ukumbi wa shule ya sekondari ya Arusha na kusisitiza kwamba kampeni hiyo ianze mara moja .
Ameiagiza ofisi ya mganga mkuu wa Jiji hilo kuhakikisha wananchi wanashirikishwa kikamilifu kupima afya zao na hataki kusikia mtu anapoteza maisha kutokana na kutokuelimishwa ili wapime homa ya Ini
Mbunge viti maalumu, Joyce Mukya,Alisema ugonjwa huo ni hatari kuliko Ukimwi hivyo Idara ya afya isifanye mchezo na ugonjwa huo kwani unaua zaidi kuliko Ukimwi .
Madiwani walisema kuwa wananchi hawana elimu juu ya ugonjwa huo ambao mpaka sasa haujawa na tiba bali tiba yake ni chanjo hivyo wananchi wakipewa elimu watachukua tahadhari na kwenda kupima afya zao kwenye vituo vya afya vya jiji la Arusha.
Akitoa ufafanuzi kaimu mganga mkuu wa Jiji la Arusha Dakta,Baraka Muondhe, alisema kuwa Chanjo iliyokuwepo awali ilikuwa ikitolewa bure kata ya Daraja mbili ,lakini sasa chanjo hiyo imekwisha na inatolewa na Zahanati binafsi .
Alisema kuwa wameshapeleka maombi ya kupatiwa Chanjo hiyo kutoka MSD na itakapopatikana itotolewa ambapo wananchi watachangia shilingi 15,000 na chanjo hiyo itatolewa kwenye vituo vyote vya afya na Zahanati za jiji la Arusha.
Wakati huohuo Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha, Karisti Lazaro, ameitaka halmashauri ya jiji hilo kuwakamata na kuwatia pingu watumishi wote watakaoonekana wanahujumu mapato ya halmashauri hiyo kwa kuwa ni mafisadi wanaokwamisha maendeleo ya jiji hilo.
Ametoa agizo hilo kwenye kikao cha robo ya mwisho yam waka 2018/19 cha baraza la madiwani alipokuwa akimpongeza mkurugenzi wa jiji hilo ,Dakta Maulid Madeni ,kwa kusimamia ukusanyaji wa mapato na hatua anazozichuku za kuwakamata watumishi wote wa halmashauri hiyo wanaojihusisha na uhujumu wa mapato .
Meya Karisti, amesema baraza hilo la madiwani linamuunga mkono kwa hatua hizo anazozichukua za kuwabana watumishi wasio waadilifu ambao ni mafisadi nakuongeza kwamba hata kama kuna madiwani ambao waashirikiana na watumishi wasio waadilifu nao wachukuliwe hatua.
Amesema kuwa mkurugenzi ameziba mianya lakini atambue kuwa hivyo ni vita kubwa lakini baraza hilo linamuunga mkono kwenye vita dhidi ya maafisa wote wanaohujumu halmashauri wapigwe pingu.
Ameipongeza halmashauri hiyo kwa kukusanya mapato kwa asilimia 105%ambapo halmashauri hiyo imekusanya shilingi bilioni 16.4 katika kipindi cha robo ya mwisho ya mwaka na hiyo inatokana na ubunifu wa kuziba mianya ya upotevu wa fedha.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa jiji ,Dakta Maulid Madeni,amesema halmashauri hiyo imechangia shilingi milioni 140 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa bara bara unaofanywa naTarura lengo ni kuzifanya bara bara zote za jiji ziwe za lami.
Amesema kuwa halmashauri haiwezi kujiondoa kwenye maswala ya utengenezaji wa bara bara ndio maana imetoa kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya kujenga bara bara hizo na kusisitiza kuwa Tarura, licha ya kuondolewa halmashauri lakini bado inawajibika kwa halmashauri hiyo.
Madiwani wakichangia wamesema kuwa Tarura, sasa tangia waondolewe halmashauri wamekuwa huru sana na hawatoi usirikiano kwa madiwani na wana urasimu na hila za ajabu ajabu .
Wamelalamikia Tarura kumrundikia kazi mkandarasi mmoja na hivyo kushindwa kutengeneza na kukamilisha barabara kwa viwango vya changarawe na moramu ziweze kupitika kwa mwaka mzima na kutaka miradi ya bara bara ifike mwisho