Wanachama 27 kutoka vyama tofauti vya upinzani kikiwemo chadema mjini Makambako mkoani Njombe wamerejesha kadi zao za awali na kuchukua kadi za chama Cha mapinduzi CCM baada ya kuridhishwa na utendaji wa viongozi wa chama kilichopo madarakani.
Wafuasi hao akiwemo Faustin Ndone wamesema wamefurahishwa na kasi ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwemo ya ujenzi wa barabara kwa kiwango Cha lami unaoendelea kote nchini,miradi ya umeme,maji,hospitali,vituo vya afya na zahanati hatua ambayo imezidi kuhimarisha upatikanaji wa huduma bora za jamii kwa wananchi.
Wamesema kuendelea kupinga jitihada za serikali iliyopo madarakani kuna fifisha dhamira ya viongozi hivyo uamuzi wa kujiunga umelenga kuunga mkono serikali iliyopo madarakani inayoongozwa na rais Magufuli.
Katika hatua nyingine wamekosoa mfumo wa utawala katika vyama vyao vya awali kwa madai ya kwamba umekosa ukweli na uwazi hali ambayo inaibua sintofahamu kwa wafuasi na wanachama wao.
Maria mgaya ni mwanachama mpya ambaye awali hakuwa na chama chochote anasema ameshawishika kuanza kujihusisha na masuala ya siasa baada ya kuridhishwa na vita dhidi ya rushwa ambayo ilikuwa tatizo kubwa na kusababisha watu kupoteza haki zao za msingi.
Akizungumza wakati wakuwapokea wanachama kutoka vyama mbalimbali vya upinzani katibu wa chama chaa mapinduzi wilaya ya Njombe Hanafi Msabaha amepongeza uamuzi wa wakujiunga na CCM kwa kuwa kupinga pinga kunawavunya moyo viongozi wliopo madarakani.
Msabaha amesema utendaji mzuri wa serikali iliyopo madarakani unakipa nafasi chama tawaala kuendelea kuaminika kwa wananchi hatua ambayo imekifanya chama hicho kuendelea kujihakikishia kushika dora katika awamu nyingine za chaguzi zijazo na kuwataka watanzania kutokuwa tayari kupokea chuki za kupandikizwa dhidi ya serikali yao.
“Sio lazima tushabikie vyama vingi ili serikali itekeleze majukumu yake kwa wananchi kwa kuwa kuna nchi kama ya Uchina ambayo inamaendeleo makubwa na imekuwa tishio kwa mataifa makubwa duniani kiuchumi likiwemo Marekani lakini bado inaongozwa na chama kimoja cha kikomunisti” Anasema Msabaha.
Katika hatua nyingine Msabaha amezungumzia suala la uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu ambapo amewataka vijana na wanawake kujitokea kugombea nafasi mbalimbali badala ya kuwaacha watu wazima na wazee kugombea nafasi hizo kwani chama kinatoa nafasi kwa rica zote.
Alex Kitalula na Damas Mahongole ambao ni viongozi wa chama cha mapinduzi katika kata ya Mji Mwema ambayo imefanikiwa kushawishi wapinzani kwa utendaji kazi wao wakizungumzia mipango yao wamesema wamejidhatiti kiutendaji ili kuondoa kabisa chembechembe za upinzani katika kata hiyo na kuahidi kuendelea kunyakua wafuasi wa upinzani.
Wamesema ujio wa jopo hilo kubwa la wafuasi waliokuwa na nguvu katika vyama mbalimbali vya upinzani unaongeza nguvu katika chama cha mapinduzi kwa kuwa watu hao watatumika kama mabarozi wakukisemea chama cha mapinduzi na kushawishi wengine kuunga mkono jitihada za serikali iliyopo madarakani.