Home Mchanganyiko SERIKALI YAWATAKA MAAFISA UGANI NCHINI KUTOA HUDUMA YA KITAALAMU KWA WANANCHI ILI...

SERIKALI YAWATAKA MAAFISA UGANI NCHINI KUTOA HUDUMA YA KITAALAMU KWA WANANCHI ILI KULETA MATOKEO CHANYA KATIKA SEKTA YA KILIMO, UVUVI NA UFUGAJI

0

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) ambaye ni Mgeni Rasmi katika
kilele cha Maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima (Nane Nane) mkoani
Kagera akielekea kukagua mabanda ya maonyesho katika Viwanja vya
Kyakailabwa mkoani Kagera. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Mhe.
Brigedia Jenerali Marco Gaguti.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) ambaye ni Mgeni Rasmi katika
kilele cha Maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima (Nane Nane) mkoani
Kagera akiangalia mboga katika shamba darasa la Jeshi la Magereza
lililopo Viwanja vya Kyakailabwa mkoani Kagera.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) ambaye ni Mgeni Rasmi katika
kilele cha Maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima (Nane Nane) mkoani
Kagera akiangalia chakula cha samaki katika bwawa la kufugia samaki la
Jeshi la Magereza Kagera lililopo Viwanja vya Kyakailabwa mkoani
Kagera.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) ambaye ni Mgeni Rasmi katika
kilele cha Maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima (Nane Nane) mkoani
Kagera akizungumza na wananchi wa mkoa wa Kagera (hawapo pichani)
katika Viwanja vya Kyakailabwa mkoani Kagera.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) ambaye ni Mgeni Rasmi katika
kilele cha Maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima (Nane Nane) mkoani
Kagera akitunuku cheti na zawadi kwa watumishi wa Kiwanda cha Sukari
Kagera ambao ni washindi wa pili wa jumla wakati wa kilele cha
Maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima katika Viwanja vya Kyakailabwa
mkoani Kagera.

**************

Serikali imewataka Maafisa Ugani nchini kutendea haki taaluma yao kwa
kutoa huduma bora ya kitaalamu kwa wananchi wanaojishughulisha katika
sekta ya kilimo, uvuvi na ufugaji ili kuwezesha upatikanaji wa maendeleo
katika sekta hizo nchini.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) alipokuwa
akifunga maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima (Nane Nane) katika
viwanja vya Kyakailabwa mkoani Kagera.

Dkt. Mwanjelwa amewasisitiza Maafisa Ugani hao kuhakikisha
wanawafuata wananchi katika maeneo yao ya uzalishaji ili kuwapatia
huduma ya kitaalamu kwa wakati badala ya kukaa ofisini.

Sanjari na hayo, Dkt. Mwanjelwa ametoa rai kwa wananchi kuzingatia
kanuni za kilimo, uvuvi na ufugaji ili kuongeza tija katika uzalishaji na
kuondokana na gharama sizizo za lazima katika shughuli za uzalishaji.

Aidha, Mhe. Dkt. Mwanjelwa amewataka wananchi kutilia mkazo katika
sekta ya kilimo kwani ndio inayobeba asilimia kubwa katika maendeleo ya
viwanda.

“Kilimo ndio sekta wezeshi kwa uchumi wa viwanda, asilimia 80 ya viwanda
vyetu inategemea malighafi ya kilimo hivyo ni lazima ipewe kipaumbele ili
kufikia uchumi wa kati wa viwanda,” Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesisitiza.

Kauli Mbiu ya Sikukuu ya Wakulima (Nane Nane) mwaka huu ni Kilimo,
Mifugo na Uvuvi kwa Ukuaji wa Uchumi wa Nchi na maadhimisho ya
kitaifa kwa mwaka huu yamefanyika mkoani Simiyu.

Dkt. Mwanjelwa amehitimisha kilele cha maadhimisho ya Sikukuu ya
Wakulima (Nane Nane) katika mkoa wa Kagera, akiwa kwenye ziara ya
kikazi kukagua utekelezaji wa shughuli za TASAF na kuhimiza uwajibikaji
kwa Watumishi wa Umma mkoani humo.