Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akipewa maelezo na Bw. Zuberi Kachingwe Afisa Usafirisahaji, IKULU,wakati Prof Palamagamba John Kabudi akikagua magari yatakayotumiwa na viongozi wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kujiridhisha juu ya matayarisho ya mapokezi ya wakuu wa Serikali na Nchi watakaohudhuria mkutano huo Dar es Salaam,Tanzania. August 8, 2019.
Bw. Zuberi Kachingwe Afisa Usafirisahaji, IKULU,(katikati) akitoa maelezo kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akikagua magari yatakayotumiwa na viongozi na Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kujiridhisha juu ya matayarisho ya mapokezi kwa ajili ya mkutano huo utakaofanyika Dar es Salaam,Tanzania. Kulia ni Afisa Usafirishaji Msaidizi Bw. Athumani Natepe. August 8, 2019.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Bw. Zuberi Kachingwe Afisa Usafirisahaji, IKULU pamoja na Bw. Athumani Natepe Afisa Usafirishaji Msaidizi mara baada ya kumaliza kukagua magari yatakayotumiwa na viongozi na Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) mkutano utakaofanyika Dar es Salaam,Tanzania. August 8, 2019.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akiwa amesimama mbele ya magari yanayotarajiwa kutumiwa na viongozi na Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kujiridhisha juu ya matayarisho ya mapokezi kwa ajili ya mkutano huo utakaofanyika Dar es Salaam,Tanzania. August 8, 2019.
Baadhi ya magari yanayotarajiwa kutumiwa na viongozi,wakuu wa Nchi na Serikali wakati wa mkutano wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) mkutano utakaofanyika Dar es Salaam,Tanzania. August 8, 2019.
**************
Serikali imesema maandalizi ya shughuli za SADC yamekamilika kwa kiwango kikubwa na sasa Tanzania iko tayari kuanza kupokea wageni na viongozi waandamizi wa Nchi 16 wanaotarajiwa kuhudhuria mkutano wa SADC unaofanyika Dar es Salaam Tanzania.
Akizungumza wakati wa ukaguzi wa magari yatakayotumiwa na viongozi mbalimbali watakaohudhuria mkutano huo wa SADC Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi amesema,maandalizi yamekamilika baada ya shughuli ya ukaguzi na kujiridhisha kuhusu utayari wa kuwapokea wageni.
Ameongeza kuwa Serikali imejiridhisha kuwa ina uwezo na iko tayari kuwapokea wageni na viongozi wakiwemo marais wa Nchi 16 za ukanda wa kusini mwa Afrika baada ya kukagua mahali watakapofikia,sehemu ya kufanyika kwa mikutano mbalimbali na mambo mengine muhimu kwa wageni hao.
Aidha,Prof. Palamagamba John Kabudi ameeleza kwa uchache utaratibu wa viongozi wakuu wa Nchi na Serikali watakavyoanza kuwasili kwa kufafanua kuwa marais na wafalme wanatarajiwa kuanza kuwasili Agust 16,2019,licha ya ukweli kuwa shughuli za SADC zimekwishaanza toka August 05,2019 ambayo ilikuwa na wiki ya maonesho ya viwanda na hii leo ni siku ya kilele ambapo Mgeni rasmi wa kufunga maonesho hayo ya viwanda atakuwa ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Mohamed Shein ikifuatiwa na mkutano wa makatibu wakuu,mawaziri na kisha wakuu wa nchi na serikali ikijumuisha Marais na Wafalme.
Katika hatua nyingine Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi na Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China Mhe. Wang Ke wamesaini hati za makabidhiano ya vifaa mbalimbali vya maofisini vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni mia mbili na kumi na saba kwa ajili ya shughuli mbalimbali za ofisini ikiwemo computer,photocopy na printerkutoka kwa Ubalozi wa Jamhuri ya watu wa China kwa ajili ya mkutano wa SADC.
Katika mkutano huu wa 39 wa Jumuia ya Maendeleo kwa Nchi za Kusini mwa Afrika SADC,Tanzania inatarajiwa kukabidhiwa kijiti cha uongozi kwa kipindi cha mwaka mmoja ambapo Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli atakuwa Mwenyekiti wa SADC.