Rais wa Zamnzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi (SMZ) Dk. Ali Mohamed Shein akimsikiliza Mshauri wa Kampuni ya ASAS Dairies Limited Bw. Abdul Ally alipokuwa akitoa maelezo wakati alipotembelea banda la kampuni hiyo katika maonesho ya nne ya wiki ya viwanda kwa nchi za Jumuiya ya Kiuchumi Kusini mwa Afrika SADC yaliyofungwa leo kwenye ukumbi wa Julius Nyerere Posta jijini Dar es salaam
Rais wa Zamnzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi (SMZ) Dk. Ali Mohamed Shein akimsikiliza Mshauri wa Kampuni ya ASAS Dairies Limited Bw. Abdul Ally alipokuwa akitoa maelezo wakati alipotembelea banda la kampuni hiyo katika maonesho ya nne ya wiki ya viwanda kwa nchi za Jumuiya ya Kiuchumi kusini mwa Afrika SADC yaliyofungwa leo kwenye ukumbi wa Julius Nyerere Posta jijini Dar essalaam
Mshauri wa Kampuni ya ASAS Dairies Limited amesema Bw. Abdul Ally kushoto akiwa na wafanyakazi wenzake katika banda hilo.
…………………………………………………..
Rais wa Zamnzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi (SMZ) Dk. Ali Mohamed Shein amishauri kampuni ya maziwa ya ASAS Dairies Limited kuhakikisha inafikisha bidhaa zake visiwani Zanzibar ili wananchi wa Zanzibar na wao waweze kuzitumia bidhaa hizo.
Rais Dk. Shein ameyasema hayo wakati alipotembelea banda la kampuni hiyo katika maonesho ya nne ya wiki ya viwanda kwa nchi za Jumuiya ya Kiuchumi kusini mwa Afrika SADC yaliyofungwa leo kwenye ukumbi wa Julius Nyerere Posta jijini Dar es salaam.
Amesema Bidhaa za maziwa ni muhimu kwa matumizi ya ya binadamu kutokana na virutubisho vyake hivyo kampuni ya ASAS itafanya jambo jema kama iitapeleka pia bidhaa hizo Zanzibar.
Naye Mshauri wa Kampuni ya ASAS Dairies Limited Bw. Abdul Ally amesema kampuni hiyo imeamua kushiriki katika Maonesho ya nne ya wiki ya viwanda kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Kiuchumi Kusini mwa Afrika SADC ili kuangalia fursa za kibiashara zilizopo katika sekta ya maziwa kwa nchi wanachama wa SADC na Africa kwa ujumla.
Bw. Allly amesema ili kufikia masoko makubwa nje ya nchi lazima kuingia kwenye soko la SADC na kutafuta fursa mpya za masoko katika jumuiya hiyo.
Alliy Amefafanua kuwa kwa sasa Kampuni ya ASAS imefanikiwa kiasi kikubwa kufikia watu wengi kwa soko la ndani pamoja na kwamba katika biashara zipo changamoto na kutafuta masoko mapya kila wakati ili kuongeza mauzo.
Amesema kampuni ya ASAS ina Uzoefu wa zaidi ya miaka 19 katika uzalishaji wa bidhaa bora za maziwa na imekuwa ikitoa huduma bora kabisa kwa wateja wake ndiyo maana bidhaa zake zinapendwa na walaji ambapo kwa sasa inazo bidhaa nyingi zikiwemo (Fresh Milk, Mtindi, Yoghurt, (Drinking yoghurt) na nyingine.
Amemalizia na kusema kuwa “Sasa Imeanza kuzalisha bidhaa mpya ya (Asas UHT Milk). Maziwa halisi ya ng’ombe aslimia 100%. yenye Uwezo wa kukaa miezi 6 nje ya jokofu (Fridge) bila kuharibika. na imetemgezwa kwa teknolojia ya kisasa”.