TIMU ya Taifa ya Tanzania ya Wanawake chini ya miaka 20 ‘Tanzanite’ leo imetinga hatua ya fainali baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya timu ya Taifa ya Afrika Kusini.
Tanzanite imealikwa kushiriki michuano ya COSAFA inayoendelea nchini Afrika Kusini na imeshinda jumla ya michezo mitatu na kupoteza mchezo mmoja.
Kwenye mchezo wa leo ambao ulikuwa na ushindani Tanzanite imeshinda mabao mawili kupitia kwa Enekia Kasonga na Opah Clement.
Itakutana na Zambia kwenye mchezo wa fainali utakaopigwa nchini Afrika Kusini.