Home Mchanganyiko RAIS WA ZANZIBAR DKT. ALI MOHAMED SHEIN AIPONGEZA MSD KWA KUKAMATA FURSA...

RAIS WA ZANZIBAR DKT. ALI MOHAMED SHEIN AIPONGEZA MSD KWA KUKAMATA FURSA ZA SADC

0

Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) Dk. Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa MSD Laurean Bwanakunu wakati alipotembelea Maonesho ya Nne ya wiki ya Viwanda kwa nchi za SADC yalifungwa leo Alhamisi Agosti 8, 2019 kwenye ukumbi wa mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.

(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWEBLOG)

Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) Dk. Ali Mohamed Shein akimueleza jambo Mkurugenzi Mkuu wa MSD Laurean Bwanakunu wakati alipotembelea Maonesho ya Nne ya wiki ya Viwanda kwa nchi za SADC yalifungwa leo Alhamisi Agosti 8, 2019 kwenye ukumbi wa mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.

Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) Dk. Ali Mohamed Shein akimsikiliza  Mkurugenzi Mkuu wa MSD Laurean Bwanakunu wakati akitoa maelezo, alipotembelea banda la MSD kwenye Maonesho ya Nne ya wiki ya Viwanda kwa nchi za SADC yalifungwa leo Alhamisi Agosti 8, 2019 kwenye ukumbi wa mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.

……………………………………………………………..
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein ameipongeza MSD kwa kuteuliwa kuwa mnunuzi mkuu wa dawa kwa ajili ya nchi za SADC.

Dkt. Shein alimweleza hayo Mkurugenzi Mkuu wa MSD Laurean Bwanakunu alipotembelea banda la MSD katika maonesho ya viwanda yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

Kingozi huyo pia ameishauri MSD kuwatembelea wazalishaji wakubwa wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara wa mataifa ili wapate taarifa sahihi na kuwashirikisha kuhusu MSD kuteuliwa kusimamia manunuzi ya pamoja ya dawa kwa nchi za SADC.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa MSD Laurean Bwanakunu amesema tayari wamejipanga vizuri kwa ajili ya manunuzi ya pamoja,ambapo tayari wameanza mchakato wa kupata wazabuni na kuanzisha mfumo wa kielektroniki utakaotumiwa na nchi wanachama kuleta mahitaji.