Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ameleta neema kwa Bohari Kuu ya Madawa Tanzania na kwa Wataalamu wa Madawa kupitia soko la uhakika la SADC.
Hayo yamesemwa na Mtendaji Mkuu wa Bohari Kuu ya Madawa Tanzania Laurian Rugambwa Bwanakunu wakati wa kuwasilisha mada ya kuonyesha mifumo mizuri ya Tanzania katika kuagiza, kutengeneza, kuhifadhi na kusambaza madawa hapa Tanzanaia. Ambayo imeifanya nchi yetu kupata tender ya kununua na kusambaza madawa katika Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika –SADC.
Akiwailisha mada katika ukumbi wa Ruaha uliopo ndani ya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere kwa wajumbe wa Maonesho ya Wiki ya Viwanda ya Nne ya SADC ambao ni wadau wa viwanda vya madawa na Wataalamu wa madawa, vitendanishi na vifaa tiba kutoka nchi 16 wananchama amesema;
“Neema tuliyoipata ya kufufua sekta ya Viwanda vya madawa, vitendanishi na vifaa tiba, kupata bajeti ya kufanya manunuzi, kuhifadhi na kusambaza dawa ni kichocheo katika kujali afya za wananchi wa Tanzania na nchi zote za SADC. Hii, imetokana na dhamira ya dhati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli ya kuweka mifumo dhabiti iliyovutia nchi za SADC na kutupa tender”
Mifumo hiyo, ni pamoja na kuandaa muongozo na muundo wa ugavi ambao umepitiwa na timu ya SADC na kupitishwa, ambapo zabuni imeshatangazwa. Kwa sasa tunategemea kupata wazalishaji wa dawa mbalimbali duniani ambao tutaingia nao mkataba ili watuuzie dawa.
Akiongea na wajumbe hao Mtendaji Mkuu Bwanakunu amesema kuwa mfumo wa taarifa wa kielektronik upo tayari, ambao utatumika kutoa taarifa za uagizaji na usambazaji wa dawa hizo katika nchi zote za SADC.
Aidha, kutokana na mjumbe kutoka Msumbiji, Malawi na Tanzania kulalamikia uwepo wa dawa zisizo rasmi ambazo zinauzwa kiholela kwa bei ya chini sana na kukosesha soko kwa dawa zilizo halali kwa matumizi. Pia, matumizi holela ya dawa kama vile antibiotic ambayo yanasababisha usugu wa vimelea vya bacteria na kuomba hatua stahiki zichukuliwe na nchi za SADC.
Akijibu changamoto hiyo Bwanakunu amesema kuwa Tanzania imechukua jukumu la kuhakikisha dawa zote zinazomilikiwa na MSD zinakuwa na alama ya kuonyesha dawa hizo ni mali ya Serikali za Tanzania (Government of Tanzania-GOT).
Akiongezea kuhusu utumiaji holela wa dawa unaosababisha usugu kwa binadamu Mkurugenzi Msaidizi wa Biashara na Viwanda vya madawa Bi Gilian Christians wa Afrika ya Kusini amesema “Nchi yangu imeanzisha madarasa ya kuelimisha jamii katika mitaa na vitongoji ambavyo wanapatikana watu wengi ili kuhakikisha elimu inayo kusudiwa inatolewa”
Alimalizia Maelezo yake Bwanakunu amesema kuwa utashi na utayari wa Tanzania katika suala la dawa umetokana na Rais Magufuli kuamua kuisimamia sekta ya madawa, vitendanishi na vifaa tiba kwa kutoa motisha na kuondoa kodi kwa wale wanaotaka kuwekeza katika eneo hilo.
Hivyo tunawakaribisha wale wote wanaotaka kuwekeza sera zetu ni nzuri na kuna mazingira mazuri ya uwekezaji Alimaliza Bwanakunu.
Naye, Rais wa Wafamasia Tanzania Issa Hango amesema kuwa tunashukuru sana Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wetu Dkt John Pombe Magufuli kwa juhudi zake za kutaka sekta ya madawa iwe kipaumbele katika kuzalisha bidhaa bora za madawa viwandani na kuwawezesha Bohari Kuu ya Madawa kwa hali na mali.
“Vikwazo vingi vilivyokuwepo katika uzalishaji na uingizaji wa malighafi vimeondolewa hakika hii imeleta neema kubwa kwa sekta ya madawa ya binadamu hapa nchini. Uwepo wa soko la uhakika la takriban watu milioni 450 wa SADC ni kichocheo kwetu kuhamasisha uwepo wa viwanda vingi na kufungua masoko mengine mbalimbali duniani”.
Tunatambua sera ya Viwanda ni jambo lililopo kwenye ajenda ya SADC, hivyo basi sisis kama wafamasia tunahitaji uwekezaji wa viwanda ambavyo vitakuwa na tekinolojia ya hali ya juu ili kuzalisha dawa zenye ubora na vigezo vinavyotakiwa Kimataifa na kuhakikisha tunaliweza soko la nchi za SADC na kwingineko duniani.
kutokana na suala la madawa kupewa kipaumbele, sasa ni wakati muafaka mitaala yetu ya vyuo kuendana na ajenda muhimu ya SADC ili kuzalisha wataalamu ambao watakidhi haja ya soko la ongezeko la viwanda vya utengenezaji wa madawa. Hii itasaidia vijana wetu wasiachwe pembeni tunahitaji kuamgalia mitaala yetu iendane na wakati. Amesema Hango
Waswahili wana msemo usemao ukishikwa shikamana, ni wakati muafaka kwa Tanzania kuhakikisha inafanikisha azma iliyokusudiwa na nchi za SADC, Aidha, uzoefu wa Tanzania katika kununua, kuhifadhi na kusambaza dawa, vifaa tiba na vitendanishi hapa Tanzania uwe kichocheo cha kufanya vema katika nchi za SADC.
Pia, mazingira wezeshi na utashi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuweka msukumo zaidi wa kuhakikisha sekta hii inafanya vizuri na kufanikiwe iwe kichocheo kwa watendaji kujituma mna kufanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha azma na jukumu ambalo Tanzania wamepewa linakamilika.
Ongezeko la Vyuo vya Fanasia hapa Tanzania liendane na mahitaji ya soko linachotaka na sio kwenda kwa mazoea ambapo tunatoa Wataalamu ambao hawakidhi vigezo vya soko la ndani na nje ya nchi.