Bw. Peter Chuwa Meneja wa Wakala wa Vipimo (WMA) Kitengo cha Bandari akizungumza na waandishi wa habari katika banda la taasisi hiyo katika maonesho ya 4 ya wiki ya Viwanda kwa nchi za SADC, Kulia ni Jared Mushi Meneja wa Viwango na Uhakiki Wakala wa Vipimo WMA na katikati ni Irene John Meneja Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma Wakala wa Vipimo (WMA)
……………………………………………………
Bw. Peter Chuwa Meneja Wakala wa Vipimo (WMA) Kitengo cha Bandari amesema Wakala wa vipimo wana kila sababu ya kushiriki katika maonesho ya 4 ya wiki ya Viwanda kwa nchi za Afrika kwa sababu nchi yetu imekuwa ikiridhia mikataba na kanuni mbalimbali zinazohusiana na masuala ya vipimo katika nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC
Peter Chuwa ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda la taasisi hiyo katika maonesho ya 4 ya wiki ya Viwanda kwa nchi za SADC yanayoendelea kwenye ukumbi wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
Amesema kwa Wakala wa Vipimo (WMA) kushiriki katika maonesho hayo kuna maana kubwa katika masuala mazima yanayohusu vipimo kwa bidhaa mbalimbali ili kumlinda mlaji katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika hasa nchini mwetu kama mwanachama wa jumuiya hiyo.
Peter Chuwa amehimiza taasisi mbalimbali kutumia Wakala wa Vipimo WMA ili kuhakiki vipimo vyao katika kulinda haki ya mlaji kupata bidhaa iliyopimwa katika vipimo sahihi na vilivyohakikiwa.
Irene John Meneja Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma Wakala wa Vipimo (WMA)akimkaribisha Bw. Peter Chuwa Meneja wa Wakala wa Vipimo (WMA) Kitengo cha Bandari ili kuzungumza na waandishi wa habari.
Bw. Peter Chuwa Meneja wa Wakala wa Vipimo (WMA) Kitengo cha Bandariakizungumza na wanahabari katika banda hilo.