***********
07/08/2019 JIJINI DAR ES SALAAM
Jeshi la Polisi nchini limetoa ufafanuzi na kuweka msisitizo kwenye katazo
alilotoa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es salaam tarehe 05/08/2019
kuhusu kupiga marufuku magari kufunga taa za vimulimuli au za rangi rangi,
taa zenye mwanga mkali (spot light) na kufunga ving’ora kwenye magari ya
kiraia au watu binafsi na pikipiki za kiraia.
Akitoa tamkoa hilo Msemaji wa Jeshi hilo SACP David Misime amesema kuwa,
katazo hilo ni kwa nchi nzima, kutokana na kujitokeza kwa baadhi ya watu
walioamua kufunga vimulimuli na ving’ora na kuvitumia wawapo barabarani
na kusababisha usumbufu kwa watumiaji wengine wa barabara. Wamefunga
vifaa hivyo kutaka kupewa kipaumbele wawapo barabarani kwa kujua au kwa
kutofahamu kuwa ni kinyume na sheria, kanuni na taratibu zilizopo.
Na Kwa mujibu wa sheria ya usalama barabarani sura ya 168 ya mwaka 1973
kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2002 kifungu cha 39 B (I) na (2)
kinafafanua juu ya matumizi ya ishara ikiwepo ving’ora na vimulimuli.