Home Mchanganyiko TAHA YAWASHAURI WADAU WA KILIMO KUCHANGAMKIA FURSA ZILIZOPO KATIKA ZAO LA RADISHI

TAHA YAWASHAURI WADAU WA KILIMO KUCHANGAMKIA FURSA ZILIZOPO KATIKA ZAO LA RADISHI

0

**************

NA GLADNESS MUSHI ARUSHA 

watanzania wameshauriwa kuchanghamkia fursa zilizopo katika zao la radishi ambalo kwa sasa lina uhuitaji mkubwa sana kwenye mahitaji ya lishe ya mwanadamu 

aidha kwa sasa zao hilo ambalo liligunduliwa  Ugiriki limeweza kuwa lishe bora  kwa makundi ya watu ambao wanauhitaji mkubwa kwa kuwa lina virutubisho vya kutosha ndani yake 
hayo yameeelzwa na Meneja mkuu wa maendeleo kutoka Asasi kilele ya wadauwa mazao ya Horticuluture Tanzania(TAHA) Bw Anthony Chamanga wakati akizungumza na “FUULSHANGWE”mapema jana kwenye viwanja vya manoesho ya wakulima na wafugaji yanayoendelea katika viwanja vya themi jijini Arusha 
Chamanga alisema kuwa zao hilo ni moja ya fursa kubwa sana hasa kwa wadau wa kilimo Tanzania kama watachamkia fursa ambazo zipo kwa kuwa mahitaji ya zao hilo ni kubwa sana 
Alisema kuwa kwa sasa zao hilo linalimwa zaidi kwenye uwanda wa juu wa bahari, mwinuko pamoja  na nyanda za juu kusini lakini pia sehemu  zenye baridi 
Alifafanua kuwa mpaka sasa wao kama TAHA wameshafanikiwa kutoa elimu kwa wakulima zaidi ya 250 ambao wanatokea katika mikoa mbalimbali na ambao wamefakiwa kulima zao hilo wanatokea katika maeneo ya Lushoto, Arusha  na Kilimanjaro 
aliongeza  kwa kusema faidia ambazo zinapatikana katika zao hilo la Radishi kuwa ni pamoja na kusaidia mmengenyo wa chakula,ianmsaidia kuzuia kansa, inaaidia kupunguza uzito, inaweza kumlinda mtu na magonwja ya kansa, pamoja na kulinda vina saba vya binadamu 
alihitimisha kwa kusema kuwa zao hilo lina weza kutumika kama tunda lakini pia likatumika katika juisi na pia hata soko au uhitaji wake ni mkubwa sana hivyo wadau wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanawasiliana na TAHA ili kupewa elimu na mbinu mbalimbali za kukuza na kuongeza zao hilo