Home Biashara Wamiliki wa viwanda vya mvinyo arusha walalamikia changamoto ya ukosefu wa zao...

Wamiliki wa viwanda vya mvinyo arusha walalamikia changamoto ya ukosefu wa zao la rozela

0

**************

Na gladness mushi arusha 

Wadau wa viwanda vya kutengeneza mvinyo kwa mkoa wa Arusha wameiomba serikali hususani sekta ya kilimo kuhakikisha kuwa wanawekeza nguvu kubwa sana kwenye mazao ya rozela ambayo ndio yanayotengeneza mvinyo .

Kwa sasa wapo baadhio ya wamiliki wa viwanda ambao wanashindwa kutengeneza mvinyo(WINE) kutokana na kukosekana kwa maligahi hiyo hali ambayo inawapa hasara kubwa sana .
Akiongea kwa niab ya wamilikki wa viwanda jijini Arusha Mkurugenzi wa kampuni ya Edmige Springs Ltd  Bi Diana mamauya alisema kuwa ipo haja ya serikali kuweka nguvu kubwa sana kwa zao hilo ambalo ni maligafi kwa viwanda hivyo 
Mamuya alisema kuwa wanalazimika wakati mwingine kusimamaisha kazi kwa ajili ya ukosefu wa rozela lakini kama wakulima wangepata msukumo mkubwa basi wangeweza kulima kwa kasi.
Alisema mahitajhi ya zao hilo kwa mkoa wa Arusha ni makubwa sana na kama wakulima wangeweza kuchangamkia fursa hiyo basi uwekezaji wa viwandaa katika zao hilo ungekuwa ni mkubwa sana .
Alifafanua kuwa kwa sasa wanahudumiwa na wakulima kutoka katika mikoa ya Dodoma wakati kwa mkoa Wa Arusha zao hilo lina stawi sana hasa katika eneo la chekereni.
Akiongealea sera ya wviwanda ya Mheshimiwa Magufuli alisema kuwa sera hiyo inatumika ipasavyoi na mpka sasa ameweza kuitekeleza kwa kuajiri wafanyakazi kama 5 ambapo kama zao hilo lingepatikana kwa uraisi basi uwekezaji ungekuwa ni mkubwa sana.