Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe.Christina Mndeme akiongea na wafanyakazi wa kampuni ya OSHA baada ya kutembelea banda hilo katika Maonesho ya Nane Nane yanayoendelea Mkoani humo
Baadhi ya wafanyakazi kutoka kampuni ya OSHA wakiweka mambo sawa kabla ya wateja kuweza kufika katika Maonesho hayo yanayoendelea Mkoani Ruvuma
Baadhi ya wateja wakiwa wanamiminika katika Maonesho ya Nane Nane yanyoendelea Mkoani Ruvuma
Mmoja wa wafanyakazi kutoka kampuni ya Osha akijaribu kumpima presha mmoja wa wateja walioweza kutembelea banda hilo katika Maonesho ya Nane Nane Mkoani Ruvuma
Baadhi ya wateja waliweza kutembelea banda la OSHA na kuweza kupata fursa ya kuelezwa kuhusu majukumu ya kampuni ya OSHA hapa nchini.
***********
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mh.Christina Mndeme ameitaka OSHA kuhakikisha suala la afya na usalama kwa mkulima kwani wakulima wengi wamekuwa hawafahamu hali ya usalama wa afya mahali pa kazi.
Akizungumza katika Maonesho ya Nane Nane yanaoendelea Mkoani Mbeya,Mh.Christina amesema kuwa wakulima wanatakiwa kufundishwa matumizi sahihi ya dhana za kilimo ili wasiweze kuumia.
“Tunataka yule mkulima anayelima mahindi anafahamu ni nini usalama wake. Niwaombe OSHA waendelee kuona elimu kwa wingi kwa wakulima kwanza kujikinga na moto”. Amesema Mh.Christina.
Aidha,Mh.Christina amesema kuwa mkulima anatakiwa kulindwa katika suala la usalama pamoja na amani hasa katika masuala ya migogoro.