******************
Serikali imewaomba wananchi, hasa wa maeneo mbalimbali nchini waanze ufugaji wa mazao ya zamani kutokana na uhitaji mkubwa wa mazao hayo duniani.
Hayo yamelezwa na Mtaalamu wa Mifugo na Uvuvi wizara wa mifugo na uvuvi katika viwanja vya Themi, jijini Arusha akitoa ufafanuzi kwa wananchi waliotembelea mabanda ya maonesho ya wakulima ( Nanenane) kanda ya Kuskazini.
Alisema serikali imekuwa ikipokea maombi mengi kutoka nchi mbalimbali duniani ya mazao ya uvuvi, hasa vyakula vinavyotokana na mazao ya bahari. Hata hivyo kiwango cha uzalishaji ni kidogo kuliko mahitaji.
Alisema mazao ya uvuvi yanasoko kubwa duniani kuliko biashara nyingine ambazo baadhi ya watu wanalazimisha kufanya, japokuwa ni haramu na kosa kwa mujibu wa sheria za nchi.
Kwakuzingatia ukweli huo,wananchi watakiwa kupata elimu ili wajikite katika ufugaji waweze kujikwamua kiuchumi na wachangie pato la taifa kupitia sekta ya uvuvi.
”Watu wanalalamika umaskini lakini kuna fursa nyingi. Sisi tunaomsaidia mheshimiwa Rais tunawajibu wakuwaonesha wananchi fursa hizo,” alisema.
Mtaalamu huyo wa wizara yenye dhamana ya uvuvi na mifugo alisisitiza kwamba mkakati wa serikali ni kuifanya nchi kuwa ya uchumi wa viwanda. Kwahiyo ili kufikia azima hiyo malighafi zinahitajika.
Ulega katika kudhihirisha wananchi watumie fursa hiyo alisema baada ya kufanikiwa kutokomeza tatizo la uvuvi haramu kwa 90%, kwahiyo sasa nimuda wa viongozi kusimamia utoaji elimu kwa wananchi kuhusu ufugaji.
Katika kuhakikisha azima hiyo inatekelezwa kikamilifu amewaagiza maofisa na wataalamu wa idara ya uvuvi waandae miradi. Kwani miongoni mwa sifa za kiongozi na mtaalamu mzuri ni uwezo wa kubuni miradi na mambo yenye tija.
Aidha Ulega amewataka viongozi na watendaji ambao maeneo yao yanashughulisha na uvuvi wahakikishe maeneo yao, hasa ya Pwani yanatumika kwa faida. Kwani maeneo hayo hayatumika kikamilifu.