Home Mchanganyiko Mamlaka ya Bandari hapa nchini yaanza utekelezaji wa miradi...

Mamlaka ya Bandari hapa nchini yaanza utekelezaji wa miradi mitatu ya bandari katika Mkoa wa Rukwa

0

aliyekuwa Meneja wa Bandari za ziwa Tanganyika (TPA)Kigoma Bw. Ajuaye Kheri Msese akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea hivi karibuni kwenye eneo la mradi mjini Kabwe  (PICHA NA MAKTABA).

………………………………………….

Na Baraka lusajo. Rukwa.

Mamlaka ya Bandari hapa nchini imeanza utekelezaji wa miradi mitatu ya bandari katika Mkoa wa Rukwa inayogharimu kiasi cha shilingi bilioni 12 .7 katika wilaya ya kalambo na Nkasi na huku serikali kupitia wizara ya ujenzi ,uchukuzi na mawasilino ikitakiwa kuharakisha ukarabati wa meli ya MV Liemba kwa lengo la kurahisisha usafilishaji wa mizigo na wananchi.

Akiongea mara baada ya kutembelea mradi ujezi wa bandari katika eneo la kipili wilayani Nkasi mkuu wa mkoa huo Joachim Wangabo , amesema wananchi wamekuwa wakiweka maisha yao hatarini kwa kutumia vyombo kama mitumbwi na boti ambavyo usalama wake ni mdogo ukilinganisha na meli kubwa ya MV Liemba ambayo usalama wake ni wa uhakika.

Naye Mbunge wa jimbo la Nkasi Kaskazini Mh Ali Kessy alieleza kuwa meli hiyo ya MV Liemba ilitakiwa kukamilishwa ukarabati wake tangu mwaka wa fedha 2017/2018 lakini fedha za ukarabati hazikutengwa na kudai kuwa Waziri wa Fedha Mh. Filipo Mpango amemuhakikishia kuwa fedha za ukarabati wa meli hiyo zimetengwa katika bajeti yam waka 2018/2019.

Kwa upande wake Meneja wa Bandari za Ziwa Tanganyika Pasivo Ntetema amesema kuwa mradi huo unahusisha ujenzi wa gati, jengo la kupumzikia abiria, jengo la mgahawa, ofisi, ghala la kuhifadhia mizigo, nyumba za wafanyakazi na uzio na kuongeza kuwa kwa Bandari ya Kabwe peke yake wastani wa usafirishaji kwa mwezi ni tani 1500 hadi 2000 na mwaka wa fedha 2018/2019 zimesafirishwa tani 20,000

“Pamoja na changamoto za miundombinu lakini utaona kuna ‘access’ nzuri ya watu kupita hapa kwahiyo kukishaboreshwa bandari hii ikakamilika lakini pia miundombinu ya barabara ya kuingia hapa ikakamilika ni Imani yetu watu wa bandari ya kwamba kupitia uongozi wako, kupitia mheshimiwa mbunge na mamlaka zote zinazotawala mkoa wa Rukwa pamoja na serikali kuu, tutaangalia sasa uwezekano wa kuboresha barabara hii kwa kiwango cha lami ili shehena kubwa iweze kupita hapa

Mamlaka ya Bandari inatekeleza miradi mitatu katika Mkoa wa Rukwa ambayo ni Mradi wa uboreshwaji wa bandari ya Kasanga iliyopo Wilaya ya Kalambo, Ujenzi wa barabara katika Bandari ya Kipili na Mradi wa Usanifu na Ujenzi wa Gati Bandari ya Kabwe zilizopo katika Wilaya ya Nkasi ambapo miradi yote itagharimu shilingi bilioni 12.7