Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akionyesha kitabu cha Bima ya Mazao wakati wa uzinduzi wa Bima ya Mazao uliofanyika kwenye Banda la NHC wakati wa maonesho ya wakulima (Nanenane) kwenye viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu, jana tarehe 4 Julai 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akimkabidhi katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe bidhaa na muongozo wa Bima ya Mazao wakati wa uzinduzi wa Bima ya Mazao uliofanyika kwenye Banda la NHC wakati wa maonesho ya wakulima (Nanenane) kwenye viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu, jana tarehe 4 Julai 2019. Mwingine Pichani (Katikati) ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka.
Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga (katikati), Mkurugenzi Mkuu wa NIC Dkt. Elirehema Doriye, akifuatiwa na Mwenyekiti wa Tume ya Ushirika Dkt.Titus Kamani, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Antony Mtaka pamoja na viongozi wengine wa sekta ya kilimo na Ushirika wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Vyama vya ushirika waliopata vyeti vya utambuzi kwa mchango katika Kilimo na Ushirika, jana tarehe 4 Julai 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akihutubia wananchi waliojitokeza wakati wa uzinduzi wa Bima ya Mazao kwenye Banda la NHC wakati wa maonesho ya wakulima (Nanenane) kwenye viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu, jana tarehe 4 Julai 2019.
Na Mathias Canal,
Wizara ya Kilimo-Simiyu
Wizara ya Kilimo-Simiyu
Katika miaka ya karibuni, Wizara ya Kilimo imebuni mbinu mbalimbali za kubadili wakulima kutoka katika kilimo cha kujikimu na kuwa cha biashara.
Kwa upande mwingine, kilimo ni biashara ye ye vihatarishi vingi kwa wakulima wa Tanzania na Bara la Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara kwa ujumla.
Hali hii imesababishwa na kutegemea mvua, mabadiliko ya hali ya hewa, moto, uharibifu wa ndege na wanyama, magonjwa ya mimea, upepo mkali, mbegu na dawa za wadudu nk. Mara nyingi, hakuna uwiano kati ya
wakulima wadogo na wakubwa katika sekta ya kilimo katika matumizi ya
teknolojia, ufikiaji wa soko, kusimamia hatari zisizodhibitiwa, utoaji wa elimu na uhamasishaji, mikopo na huduma za
bima.
wakulima wadogo na wakubwa katika sekta ya kilimo katika matumizi ya
teknolojia, ufikiaji wa soko, kusimamia hatari zisizodhibitiwa, utoaji wa elimu na uhamasishaji, mikopo na huduma za
bima.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo jana tarehe 4 Julai 2019 wakati akizundua Bima ya Mazao ambapo alisisitiza kuwa, kuanzisha Bima ya Mazao ni muhimu kwa wakulima nchini Tanzania ili kukabiliana na hasara zitokanazo na vihatarishi vinavyoathiri uzalishaji.
Mhe Hasunga alisema kuwa kuna kampuni kadhaa za Bima
ambazo zimeanzisha bidhaa mbalimbali za bima kwa ajili ya kumkinga mkulima dhidi ya hasara kwa aina tofauti za mazao. Kampuni hizo ni pamoja na Kampuni ya Bima ya Taifa (NIC), Jubilee na UAP.
ambazo zimeanzisha bidhaa mbalimbali za bima kwa ajili ya kumkinga mkulima dhidi ya hasara kwa aina tofauti za mazao. Kampuni hizo ni pamoja na Kampuni ya Bima ya Taifa (NIC), Jubilee na UAP.
Hata hivyo, utoaji wa bidhaa za bima ya mazao umekuwa ukifanyika bila mwongozo thabiti ambao ungewanufaisha wakulimna wengi wadogo hususan maeneo ya vijijini. Hivyo, mwongozo huu unaolenga kubainisha namna bima ya mazao inavyoweza kuwakinga wakulima dhidi ya hasara una umuhimu wa kipekee kwa wakati huu wa mapinduzi makubwa ya sekta ya kilimo nchini.
Alisema kuwa Bima ya mazao aliyoandaliwa na NIC kwa kushirikiana na Wizara ya kilimo iliyozinduliwa ni faraja kubwa kwa wakulima nchini.
Uandaaji wa Bima ya mazao iliyozinduliwa pamoja na Mwongozo vimezingatia: Dira ya Maendeleo ya Taifa (Tanzania Development Vision 2025); Mpango wa Taswira ya Muda Mrefu wa Taifa (Long Term Perspective Plan -LTPP 2012-2021); Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano (Five Year Development Plan II – FYDP II 2016-21); Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili (Agricultural Sector Development Program II – ASDP II ). Vilevile, Sheria ya Bima Namba 10 ya mwaka 2009 (Tanzania Insurance Regulatory Authority Act. No. 10 of 2009) imezingatiwa.
Mhe Hasunga amesema kuwa Miongoni mwa manufaa yapatikanayo kutokana na kuwepo kwa mwongozo wa Bima ya Mazao ni pamoja na kutoa fursa kwa wakulima kupata aina sahihi ya bidhaa ya bima ya mazao kutoka kwa kampuni za bima zenye vibali na zilizosajiliwa, kuwapa wakulima uwezo wa kuchagua aina ya bima ya mazao waipendayo, na kuwezesha wakulima kubadili tabia ili kufuata kanunu bora za kilimo.
Zingine ni kudhibiti kampuni zinazotoa huduma za bima ya mazao ili kubuni bidhaa za bima ya mazao ambazo zina manufaa makubwa kwa wakulima, kujenga uaminifu miongoni na taasisi za fedha kwa kutoa mikopo ya kilimo na kuweka mazingira wezeshi kwa wakulima katika taratibu za kujiandikisha, kuwasilisha madai, kinga ya mazao na taratibu za malipo pindi hasara inavyotolewa taarifa.
Kadhalika Mhe Hasunga alisema kuwa utekelezaji wa Mwongozo huo kwa ukamilifu, utawezekana ikiwa kutakuwa na juhudi za pamoja kati ya Wizara ya Kilimo na wadau wengine wanaojishughulisha na kilimo cha mazao ya chakula na biashara.
Alisema Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, imeendelea kuimarisha na kuendeleza ukuaji wa Sekta ya Kilimo Nchini kutumia programu mbali mbali kwa kushirikiana na wabia wa maendeleo ya kilimo.
Uendelezaji wa sekta hii ya kilimo ni muhimu katika kuchochea ukuaji wa uchumi wa Taifa, unaopelekea ukuaji wa sekta ya viwanda, upatikanaji
wa chakula na lishe ya kutosha kwa Watanzania na uzalishaji wa kibiashara. Kwa sasa, sekta ya kilimo inachangia 29.1% ya Pato la Taifa, 65.5% ya ajira, 65% ya malighafi za sekta ya viwanda na 30% ya mapato yatokanayo na mauzo ya nje ya nchi.
wa chakula na lishe ya kutosha kwa Watanzania na uzalishaji wa kibiashara. Kwa sasa, sekta ya kilimo inachangia 29.1% ya Pato la Taifa, 65.5% ya ajira, 65% ya malighafi za sekta ya viwanda na 30% ya mapato yatokanayo na mauzo ya nje ya nchi.