*************
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda ametangaza kuwa ifikapo August 06 atafunga Barabara zinazozunguka Chuo cha IFM zenye ukubwa wa Mita 700 ili eneo hilo litumiwe na Wachonga vinyago, Wachoraji wa picha na watengeneza Shanga kuuza bidhaa wanazozalisha kwa
ndani ya siku 15 za ugeni wa viongozi wa Jumuiya ya SADC.
RC Makonda amesema kwakuwa eneo hilo lipo jirani na Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere unapofanyika mkutano huo itakuwa rahisi kwa wageni kutembelea wafanyabiashara hao na kununua bidhaa mbalimbali zinazatengenezwa kwa umahiri na ubunifu mkubwa ikiwemo Vinyago, Picha za kuchora, Shanga na Vinyago jambo litakalosaidia pia kutangaza utalii wa Tanzania.
Aidha RC Makonda amesema eneo hilo pia litakuwa na ulinzi wa kutosha na litafungwa Taa za kisasa ili kuhakikisha wageni wafika na kununua bidhaa muda wowote kwa kipindi chote cha mkutano wa Jumuiya ya SADC jambo litakalosaidia kukuza uchumi wa wauzaji na Taifa kwa ujumla.
Hata hivyo RC Makonda amesema ni vyema Wananchi wakauchukulia Ugeni huu wa Viongozi zaidi ya 16 wa Jumuiya ya SADC kama sehemu ya fursa ya kuuza na kutangaza bidhaa zao.