Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya magari ya AMC (Nissan) Tanzania, Bw. Christophe Henning akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na msaada waliotoa shule ya Viziwi Buguruni ikiwa ni sehemu ya kurudisha faida kwa jamii kutokana na biashara wanayoifanya hapa nchini
wakati wa hafla fupi iliyofanyika shule ya Viziwi Buguruni jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya magari ya AMC (Nissan) Tanzania, Bw. Christophe Henning (wa pili kulia) pamoja na Mwalimu Mkuu wa shule ya Viziwi Buguruni, Bi. Kulwa Milembe (wa pili kushoto) wakimkabidhi mwanafunzi Abdilahi Akida zawadi ya begi lenye daftari pamoja na kompasi wakati wa hafla fupi iliyofanyika shuleni hapo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja Masoko na Mauzo wa Kampuni ya magari ya AMC Tanzania, Bw. Alfred Minja na Afisa mauzo wa kampuni hiyo, Bw. Hussein Khalfan (kulia) wakishuhudia tukio hilo.
Meneja Masoko na Mauzo wa Kampuni ya magari ya AMC Tanzania, Bw. Alfred Minja akitambulisha msafara wake aliombatana nao shuleni hapo akiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya magari ya AMC (Nissan) Tanzania, Bw. Christophe Henning wakati wa hafla fupi ya kukabidhi msaada wa mabegi na kompasi iliyofanyika shuleni hapo jijini Dar es Salaam.
Pichani juu na chini ni Afisa Masoko Msaidizi wa Kampuni ya magari ya AMC (Nissan) Tanzania, Bi Angelina Ndege akiendelea na zoezi la kukabidhi msaada wa mabegi na kompasi kwa wanafunzi wa shule ya Viziwi Buguruni wakati wa hafla fupi iliyofanyika shuleni hapo jijini Dar es Salaam
Wanafunzi wa shule ya Viziwi Buguruni wakipata chakula cha mchana kilichoandaliwa na Kampuni ya magari ya AMC (Nissan) Tanzania wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa mabegi na kompasi fupi iliyofanyika shuleni hapo jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya magari ya AMC (Nissan) Tanzania, Bw. Christophe Henning akisalimiana na wanafunzi pamoja na walimu (hawapo pichani) wa shule ya Viziwi Buguruni wakati wa hafla fupi ya kukabidhi msaada wa mabegi na kompasi iliyofanyika shuleni hapo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya magari ya AMC (Nissan) Tanzania, Bw. Christophe Henning (wa pili kulia) pamoja na Mwalimu Mkuu wa shule ya Viziwi Buguruni, Bi. Kulwa Milembe (wa pili kushoto) wakimkabidhi mwanafunzi Hanifa Mrisho zawadi ya begi lenye daftari pamoja na kompasi wakati wa hafla fupi iliyofanyika shuleni hapo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja Masoko na Mauzo wa Kampuni ya magari ya AMC Tanzania, Bw. Alfred Minja na Afisa mauzo wa kampuni hiyo, Bw. Hussein Khalfan (kulia) wakishuhudia tukio hilo.
Mwalimu Mkuu wa shule ya Viziwi Buguruni, Bi. Kulwa Milembe akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu furaha yao kwa ujio wa Kampuni ya magari ya AMC (Nissan) Tanzania shuleni hapo wakati wa hafla fupi ya kukabidhi msaada wa mabegi na kompasi iliyofanyika shuleni hapo jijini Dar es Salaam.
***********
Nissan yapeleka furaha shule ya Viziwi Buguruni
Na Mwandishi wetu
KAMPUNI ya magari ya AMC Tanzania imepeleka furaha shule ya Viziwi Buguruni baada ya kukabidhi uongozi wa shule bidhaa mbalimbali kwa ajili ya wanafunzi 237 wanasoma katika shule hiyo.
Kampuni ya AMC Tanzania ndio wauzaji pekee wa magari aina ya Nissan nchini.
Akikabidhi vifaa hivyo, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya AMC Tanzania, Christophe Henning amesema kwamba wamejisikia fahari kusaidia wenye mahitaji.
Aidha alisema kwamba kampuni yake itakaa katika meza tena na uongozi wa shule hiyo kuona namna ya kuisaidia shule hiyo.
Kampuni ya AMC TANZANIA ambayo kwa sasa inatimiza miaka mitano tangu kufunguliwa nchini imesema kwamba inafanya hisani hiyo kurejesha faida kwa wananchi.
“Kama sehemu ya wajibu wetu wa kurejesha faida kwa wananchi tumeona tujikite kusaidia wenye mahitaji hasa watoto ili waweze kupata elimu katika maizngira bora kwani tunaamini viwili (watoto na elimu) hivyo ni muhimu katika maendeleo ya nchi.” alisema Henning.
Kampuni hiyo miongoni mwa bidhaa walizowapa wanafunzi ni mabegi na kompasi.
Alisema kwamba kampuni ya Nissan ambayo inatengeneza mitambo mbalimbali inajivunia kauli mbiu yake ya ubunifu unaofurahishwa ambao umewafanya kuwa moja ya makampuni ya kutumainiwa duniani na yanayofanya biashara vyema.
Alisema kutokana na bishara zake wanapata nafasi ya kurejesha faida kwa jamii kwa kuwekeza zaidi kwa watoto wenye mahitaji na elimu yao.
Nissan ambao kwa sasa wapo Plot No. 6, Vingunguti Area, Nyerere Road na kuwa na matawi katika miji mikuu ya kibiashara nchini kama Arusha, Dodoma, Zanzibar, Mwanza, Mbeya na Morogoro.
Katika hotuba yake mtendaji huyo aliahidi Nissan Tanzania kuendeleza ushirikiano na shule ya Buguruni kwa manufaa ya pande zote mbili ili kuleta ustawi katika jamii.
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Kulwa Milembe akishukuru kwa zawadi hizo alisema kwamba wanafunzi wake wanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwamo vifaa vya kubebea vitu wanafunzi ambao wengine wametoka nje ya Dar es salaam na familia zao ni duni sana.
Alisema wanafunzi wengi wamekuwa hawana vibebeo vya madaftari, kwa hiyo msaada wa mabegi ni tunu kubwa kwao.
Alisema pamoja na msaada huo atapenda kampuni hiyo kuendelea kusaidia wanafunzi wake ili waweze kusonga mbele katika elimu. Shule hiyo yenye wavulana 110 na wasichana 127 na kufanya jumla yao kuwa 237 ina vitengo vya
msingi, ufundi, awali na wasioona.