katika kuwezesha sekta mbalimbali za maendeleo nchini
ambapo katika maonesho ya mwaka huu ya nane nane
ambayo kitaifa yanaadhimishwa mkoani Simiyu Benki hiyo
imekuja na kauli mbiu ya “Kilimo chetu, Viwanda vyetu, Uchumi
wetu”.
Akizungumza katika maonesho hayo ambayo yamezinduliwa
rasmi leo hii na Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan,
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Boma Raballa
alisema Benki ya CRDB inaamini kuwa uwezeshaji wa sekta ya
kilimo utasaidia kuongeza malighafi katika viwanda nchini na
hivyo kuchochea ukuaji wa uchumi wa taifa.
“Tukiwa Benki ya kizalendo nchini tupo tayari kushirikiana na
Serikali yetu kujenga uchumi wa kati unaoshamirishwa na
viwanda. Ambavyo kwa uhalisia vinategemea sana mazao ya
kilimo kama malighafi zake,” alisema ndugu Boma Raballa.
Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe aliipongeza Benki ya
CRDB kwa kuwa mstari wa mbele kuwezesha sekta ya kilimo
kupitia huduma na bidhaa mbalimbali inazozitoa Benki hiyo
kwa ajili ya kilimo ikiwamo mikopo ya pembejeo za kilimo.
“Nimefurahishwa sana na kauli mbiu yenu ya ‘Kilimo Chetu,
Viwanda Vyetu, Uchumi wetu’ hii inaonyesha ni jinsi gani Benki
hii imejipanga vilivyo kuboresha sekta hii muhimu ambayo ni
kichocheo kikubwa katika kufikia uchumi wa kati wa viwanda”,
alisema Hussein Bashe.
Akimueleza Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe juu ya
mchango wa Benki ya CRDB katika maendeleo kilimo nchini
ndugu Boma Raballa alisema Benki ya CRDB inatoa zaidi yaasilimia 40% ya mikopo yote itolewayo kwa ajili ya kilimo nchini.
Ambapo kwa kipindi cha mwaka 2018/2019, zaidi ya shilingi
bilioni 650 zimeshatolewa. Katika hizo, shilingi bilioni 150 yaani
asilimia 23% , zimeelekezwa katika kilimo cha mazao ya
biashara na malighafi za viwanda, utengenezaji wa pembejeo,
usindikaji na usambazaji.
Raballa alisema pia Benki ya CRDB imekuwa
ikishirikiana na kwa karibu wadau wadau mbalimbali wa sekta
ya kilimo nchini ikiwamo Benki Kuu ya Tanzania, Benki ya
Maendeleo ya Kilimo (TADB), Shirika la Uwezeshaji wa Kilimo
(PASS), Mfuko wa Afrika Gurantee (AGF), Shirika la
Uwezeshaji Kifedha la Kimataifa (IFC), Benki ya Maendeleo
Afrika (AFDB), Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO),
Ushirikiano wa Maendeleo ya Viwanda (IDC) na Kampuni ya
ETC Agro katika kuwawezesha wakulima nchini kupitia
mafunzo mbalimbali juu ya ufahamu wa masuala ya fedha,
uwekezaji , utafutaji masoko na mikopo ya kilimo.
wakati alipotembelea banda la Benki ya CRDB katika maonyesho ya 26 ya kilimo na mifugo (Nane Nane 2019), yaliyofunguliwa rasmi leo na Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan
kwenye viwanja vya Nyakabindi, Mkoani Simiyu. Katikati ni Mkurugenzi wa Wateja wa Kati na Wadogo wa Benki ya CRDB, Boma Raballa.
—