Baada ya klabu ya Yanga kuzindua wiki ya mwananchi siku nne zilizopita ambayo itatumika kufanya shughuli za kijamii katika maeneo mbalimbali nchini, Katika mkoa wa Njombe wapenzi na mashabiki timu hiyo mjini Makambako wameanza utekelezaji wa malengo ya wiki hiyo kwa kufanya usafi na kutoa misaada kwa wagonjwa katika hospitali ya mji wa Makambako.
Wanachama hao na wapenzi wa klabu ya Yanga wamesema wamehamasika kufanya hivyo baada ya kuridhishwa na mwenendo wa klabu yao pendwa pamoja na taarifa ya kurudi kwa kocha kipenzi cha mashabiki Mwinyi Zahera ambaye walikuwa na hofu ya kutorejea nchini kwa madai yakuzushiwa ya kwamba hajalipwa mishahara hivyo anamgomo.
Wakizungumza mara baada ya kufanya matembezi ya viunga mbalimbali vya mji wa Makambako kuelekea hospitali ya mji huo ambayo yamefanyika huku vijembe vikipigwa kwa watani wao Simba mashabiki hao wamesema kwa usajiri na maandalizi ambayo yamefanywa na klabu hiyo wanahakika wanaenda kubeba ubingwa wa ligi na klabu bingwa huku wakitoa tahadhali kwa timu ya mbao,Lipuli na mtani kupigwa hamsa kila wanapokutana nao.
Akieleza sababu ya kuchagua kuwatembelea wagonjwa katika wiki ya Mwananchi mwenyekiti wa tawi la Yanga mjini Makambako David Nyika na Hitra Msola msemaji wa tawi wamesema wafanya hivyo ili kuunga mkono jitihada za mwenyekiti wa klabu na kuwataka wanachama wa Yanda Tanzania nzima kuendelea na mpango wa kuichangia klabu ili kupata fedha za kulipa mishahara wachezaji na viongozi
Dr Ivan Fute kaimu mganga mkuu hospitali ya mji wa Makambako na Edafina Kigosi muuguzi mkuu wodi ya akina mama wanatoa shukrani kwa mashabiki wa klabu ya Yanga na kutoa wito kwa vilabu vingine kuiga mfano huo.
Baada ya kuhitimisha zoezi la usafi na kutoa msaada kwa wagonjwa mwenyekiti wa tawi la makambako DAVID NYIKA anapewa heshima ya kuzindua shina la yanga na kupandisha bendera