Operesheni ya usiku na mchana ya udhibiti wa utoroshaji wa mapato iliyoongozwa na mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafiri imezaa matunda katika halmashauri ya wilaya ya Njombe baada kufanikiwa kudhiti mianya yote ya rushwa,utoroshaji wa mapato na kuifanya halmashauri hiyo kuvuka lengo la ukusanyaji mapato kwa asilimia 115 katika 2018/2019.
Zoezi hilo ambalo lilifanyika kwa kufanya doria za kushitukiza nyakati za usiku na mchana katika maeneo tofauti ya wilaya ya Njombe na kuongeza vizuizi katika kata na vijiji limefanikiwa kwa kiasi kikubwa na kuleta matokeo chanya kwa kuwa wakepaji wa mapato hususani wafanyabiashara wa mbao wamebadilika na kuanza kutii sheria zilizopo jambo ambalo limeleta faraja kimapato.
Penye mafanikio panatajwa kuwa na vikwazo vingi na hapa mtandao huu unazungumza na baadhi ya watendaji wa kata akiwemo….ambao wanasema wamekuwa wakipokea vitisho naushawishi wa rushwa kutoka kwa wafanyabishara wakubwa na kuzikataa jambao ambalo linatengeneza chuki na usalama mdogo kwa watendaji
Nao baadhi ya madiwani akiwempo Shaibu Masasi na Daina Mangula wanasema mafanikio yaliopatikana yametokana na jitihada kubwa za kikosi kazi cha udhuibiti,ongezeko la vizuizi pamoja na ushirikiano mkubwa baina ya watendaji huku pia wakipongeza hatua ya halmashauri ya kutekeleza mradi mmoja katika kila kata kupitia mapato ya ndani itaongeza imani kwa wananchi ya kulipa ushuru
Aidha madiwani hao wamesema wamejidhatiti kiulinzi na kuongeza ubunifu wa miradi mipya ya maendeleo ili mwaka mpya wa serikali waweze kuongeza kiwango cha ukusanyaji zaidi ya mwaka huu .