Home Mchanganyiko VIJANA WAKISHIRIKI IPASAVYO KWENYE KILIMO UCHUMI UTAIMARIKA-MHE HASUNGA

VIJANA WAKISHIRIKI IPASAVYO KWENYE KILIMO UCHUMI UTAIMARIKA-MHE HASUNGA

0

Mbunge wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo akisisitiza jambo wakati akizungumza na vijana wa Jimbo la Vwawa katika kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa Chama Cha Mapinduzi makao makuu ya Chama hicho Wilayani Mbozi, leo tarehe 28 Julai 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)

Vijana wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe wakimsikiliza kwa makini Mbunge wa Jimbo hilo ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga wakati akizungumza katika kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa Chama Cha Mapinduzi makao makuu ya chama hicho Wilayani Mbozi, leo tarehe 28 Julai 2019.

Mbunge wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo akiagana na vijana wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe mara baada ya kikao na vijana hao kilichofanyika katika ukumbi wa Chama Cha Mapinduzi makao makuu ya Chama hicho Wilayani Mbozi, leo tarehe 28 Julai 2019.

Mbunge wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo akisisitiza jambo wakati akizungumza na vijana wa Jimbo la Vwawa katika kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa Chama Cha Mapinduzi makao makuu ya Chama hicho Wilayani Mbozi, leo tarehe 28 Julai 2019.

 

Na
Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Songwe

Mbunge wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe ambaye ni
Waziri wa Kilimo anakusudia kuwakutanisha vijana kwa ajili ya kongamano la
kujadili fursa zilizopo katika sekta ya Kilimo.

Waziri Hasunga ameyasema hayo tarehe 28 Julai 2019
wakati akizungumza na vijana wa Jimbo la Vwawa katika kikao kazi kilichofanyika
katika ukumbi wa Chama Cha Mapinduzi makao makuu ya Chama hicho Wilayani Mbozi.

Alisema kuwa zaidi ya asilimia 70 ya watanzania
wanajihusisha na Kilimo lakini miongoni mwao vijana ni wachache hivyo mkakati
huo wa kuwakutanisha vijana ni sehemu ya kueleza kwa viajan fursa zilizopo
kwenye sekta ya Kilimo na kuziendeleza.

Alisema kuwa vijana ndio nguvu kazi ya Taifa hivyo
kuhusishwa kwenye sekta ya Kilimo ni miongoni mwa mambo msingi yatakayoinua
uchumi wa vijana nchini kadhalika kuimarisha uchumi wa Taifa.

Mhe Hasunga amesema kuwa vijana wengi wamekuwa
wakijihusisha na mambo yasiyokuwa na tija katika Jamii kama vile kushinda
vijiweni badala yake wanatakiwa kufanya kazi kwa bidii ili kuimarisha kipato
chao kitakachopelekea vijana kutojihusisha na uovu wa aina yoyote.

Kuhusu kuimarisha masoko ya mazao mbalimbali
ikiwemo zao la kahawa, Mhe Hasunga amesema kuwa tayari wizara ya kilimo
imeanzisha mkakati kabambe wa kuongeza minada ya kahawa ambapo kwa upande wa
Kanda ya ziwa mnada utafanyika mkoani Kagera, Kanda ya Kaskazini utafanyika
Manispaa ya Moshi, Kanda ya kusini utafanyika wilayani Mbinga na Kanda ya
nyanda za juu kusini mnada wa kahawa utafanyika Wilayani Mbozi.

Ameongeza kuwa kuongeza minada ya uuzaji wa zao la
kahawa utatoa fursa kwa wakulima kunufaika na mazao yao kwa kuuza kwa bei nzuri
na kulipwa kwa wakati.

Mhe Hasunga amewasihi wakulima mkoani Songwe na
Taifa kwa ujumla wake kujishughulisha zaidi na Kilimo kwani ndio sehemu pekee
yenye uwezo wa kuwaongezea kipato chao.

Kuhusu kadhia ya mbegu feki kwa wakulima Mhe
Hasunga amesema kuwa serikali imejipanga kuimarisha upatikanaji wa viuatilifu
kwa wakati na kwa bei nafuu ili wakulima waweze kuvimudu.

“Kumekuwa na mbegu nyingi mtaani ambazo sio
sahihi kwa maana hiyo sasa serikali inachukua hatua kali kwa wafanyabiashara
wanaojihusisha na biashara hiyo punde watakapobainika” Alikaririwa Mhe
Hasunga