Home Mchanganyiko UTOMVU NI DHAHABU NYINGINE INAYOPATIKANA KATIKA SHAMBA LA SAO HILL

UTOMVU NI DHAHABU NYINGINE INAYOPATIKANA KATIKA SHAMBA LA SAO HILL

0

Mkurugenzi wa Rasilimali Misitu na Nyuki TFS, Zawadi Mbwambo akitoa maelezo jinsi gani wanavyovuna utomvu kwa baadhi ya viongozi wa wilaya ya Chato,Mkoa wa Geita na viongozi wa vijiji vinavyolizunguka Shamba la Miti la Biharamulo lililopo mkoani Geita baada ya kutembelea Shamba la Miti Sao Hill linalosimamiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kwa lengo la kujifunza shughuli mbalimbali za uendeshaji katika shamba hilo.

Baadhi ya viongozi wa wilaya ya Chato,Mkoa wa Geita na viongozi wa vijiji vinavyolizunguka Shamba la Miti la Biharamulo lililopo mkoani Geita wakishangaa jinsi miti inavyoweza kutoa mabilioni ya fedha baada ya kutembelea Shamba la Miti Sao Hill linalosimamiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kwa lengo la kujifunza shughuli mbalimbali za uendeshaji katika shamba hilo

Moja kati ya maeneo ya Shamba la Miti Sao Hill linalosimamiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) NA FREDY
MGUNDA,IRINGA.

 

Watanzania kuanza
kunufaika na zao la miti kutokana na uvunaji wa utomvu kutoka kwenye miti ya
kupandwa iliyopo kwenye Shamba la Sao Hill lililopo Mufindi mkoani Iringa kwa
kuiliingizia taifa zaidi ya shilingi bilioni mbili kwa kupindi cha miaka miwili
ya majaribio.

 

Hiyo imebainika
wakati wa ziara ya baadhi ya viongozi wa wilaya ya Chato,Mkoa wa Geita na
viongozi wa vijiji vinavyolizunguka Shamba la Miti la Biharamulo lililopo
mkoani Geita baada ya kutembelea Shamba la Miti Sao Hill linalosimamiwa na
Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kwa lengo la kujifunza shughuli
mbalimbali za uendeshaji katika shamba hilo
.

 

Akitoa ufafanuzi
mkurugenzi wa Rasilimali Misitu na Nyuki TFS, Zawadi Mbwambo alisema kuwa Shamba
la Miti Sao Hill wameanziasha mradi mpya wa kuvuna utomvu ambao umekuwa
unatengenezewa gundi kwa ajili ya kutumika kwenye bidhaa mbalimbali kulinga na
mahitaji ya wahusika.

 

“Tumeanza kugema
utomvu kwenye miti mikubwa kwa kuwa tupo kwenye majaribia lakini wataalamu
wamesema kuwa ukianza kugema utomvu mti ukiwa na umri mdogo basi utagemwa kwa
muda mrefu na kuleta faida kwa wananchi na taifa kwa ujumla, na kumbukeni kuwa
hapa mti haukatwe unaendelea kustawi tu” alisema Mbwambo

 

 

Mbwambo
alisema kuwa takwimu za dunia zinaonyesha kuwa inawezekana utomvu ukawa unalipa
zaidi ya zao la miti hivyo utafiti ukimalizika yawezekana wakulima wa miti
wakahamia kwenye uvumaji wa utomvu.

 

“Kwa takwimu
hizo sio muda faida kubwa itakuja kwa wananchi na serikali kwa ujumla maana
inaonyesha dhahili kuwa utomvu unalipa sana kuliko mbao hiyo watafiti waliopo
hapa katika shamba la Sao Hill ukizaa matunda basi utahamia kwa wakulima wa
miti” alisema Mbwambo

 

Mbwambo
alisema kuwa miti milioni tatu kila mwaka ndio inatumika katika uvunaji wa
utomvu na hakuna eneo maalum ambao limetengwa kwa ajili ya kuvuna bali wametoa
maeneo ambayo yanamiti ambayo inatarajiwa kuvunwa baada ya miaka miwili ijayo

 

“Shamba hili
la Sao Hill ni kubwa sana linakaribia kuwa na hekta laki moja na elfu hamsini
na nne hivyo sio rahisi kufanya majaribio shamba lote hiyo tumetoa eneo ambalo
miti yake inatarajiwa kuvunwa baada ya miaka miwili” alisema Mbwambo

 

Mbwambo
alisema kuwa soko la utomvu duniani kwa sasa linategemee kutoka nchi China
hivyo soko lipo huko na kampuni ya AATY Limited ya kichini inavyovuna hapa
katika shamba la Sao Hill na ni kampuni kubwa kuliko zote dunia za uvunaji wa utomvu
duniani.

 

 

Akizungumza
kwenye eneo la tukio mkuu wa msafara huo Mkuu wa Wilaya ya Chato Mhe. Eng.
Mtemi Msafiri alisema kuwa wamejifunza kitu kipya ambacho hawakuwahi
kukifikiria katika maisha yao kuwa uvunaji au ugemaji wa utomvu unalipa kwa
namna hiyo.

 

“Navyo sema
kuwa sasa tumegundua dhahabu ya kijani namaanisha hivi,utomvu unaigiza fedha
nyingi tumeana hapa mkurugenzi katueleza hivyo ni lazima tuchukue swala hili
kwa umuhimu stahili ili hata kweli kwetu Chato tutalifanya kwa umakini mno”
alisema Msafiri

 

Shamba la
Sao Hill lililopo hapa Mufindi lilianzishwa kwa majaribio mnamo mwaka 1939 hadi
mwaka 1951 na upandaji kwa kiasi kikubwa ulianza rasmi mwaka 1960 hadi 1980 na
shamba hilo linaukubwa wa hekta 135,903 ambazo zimehifadhiwa kwa ajili ya
upandaji wa miti na uhifadhi wa mazingira na shamba hilo ni miongoni mwa
mashamba 23 ya miti ya kupandwa ya serikali ambayo yanasimamiwa na wizara ya
maliasili na utalii kupitia Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS).